Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesema hakuja kwa kimbunga katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwani amekuzwa, kujengwa na kukulia katika chama hicho.
Amesema ana amini katika malengo makuu ya taasisi, Demokrasia, Uhuru wa watu, uchumi shirikishi, elimu bora na bure,”
Aliendelea kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa anaamink katika bunge lenye nguvu na uwezo wa kusimamia serikali, utawala wa sheria na haki.
Sikuja kwa kimbunga Chadema, nimekuzwa, nimejengwa na kukulia humu...naamini katika malengo makuu ya taasisi, naamini katika demokrasia, uhuru wa watu, uchumi shirikishi, Elimu bora na bure,naamini katika bunge lenye nguvu na uwezo wa kusimamia serikali,utawala wa sheria na haki. pic.twitter.com/3Ard167CV1— John Heche (@HecheJohn) February 20, 2020