Mbunge SUGU Atoa Mpya.."Chadema Inashinda Ubunge MBEYA Bila Hata ya Tume Huru"



Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi maarufu 'Sugu' amesema atagombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 na ana uhakika ataibuka mshindi

Amesema, "Kuna wanaoniuliza kama nitagombea. Nataka niwaambie nitagombea, siyo kugombea tu bali nitashinda. Kuwe na tume huru ya uchaguzi au isiwepo."

Ameeleza hayo jana Jijini Mbeya na kusisitiza kuwa CHADEMA lazima ishinde Jiji la Mbeya kwa sababu watahakikisha kura zinapigwa na watazilinda

Aidha, amebainisha kuwa kuhama kwa Madiwani 11 wa CHADEMA katika Jiji la Mbeya kwenda CCM hakuwezi kubadili mapenzi ya Wananchi wa Mbeya kwa CHADEMA

Madiwani hao walipokelewa Jumatatu na Dkt. Bashiru katika ofisi za CCM Jijini Dodoma huku Bashiru akisema hizo ni salamu kwa Sugu kuelekea Uchaguzi Mkuu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad