Mchomvu Awafungukia Diamond, AliKiba Amtaja Mr Blue



MTANGAZAJI wa kipindi cha XXL cha Clouds Fm na Mwanamuziki, Adam Mchomvu, jana amefanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio iliyopo katika mjengo wa Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam ambapo amefungukia mambo mbalimbali ikiwemo muziki wake, maisha yake pamoja na kazi yake ya utangazaji.

 

Akifanya mahojiano na kipindi hicho, Mchomvu amesema watangazaji ni watu wanaojua burudani na endapo angepewa nafasi ya kutoa tuzo kwa msanii wa Bongo Fleva, angempa Mr Blue kwani ni msanii aliyenza muziki akiwa mdogo, ana nidhamu ya hali ya juu na bado anaendelea kufanya vizuri.



Kwenye mahojiano hayo, Mchomvu aliizungumzia pia Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli.



“Ningependa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, Magufuli anatisha sana kaja kapindua, kidogo nidhamu inakaa, tunaenda lakini bado kwenye nyimbo nyimbo huku, kuna kuchochea mambo ya mapenzi zaidi,” alisema Mchomvu.



Alipoulizwa kuhusu uwezo wa Diamond na mchango wake katika Bongo Fleva, Mchomvu alisema:

“Honestly Diamond amefanya kitu kikubwa sana, na ni mmoja kati ya ma-game changer, kaibadilisha sanaa, ameiweka kwenye Map, dunia inaijua Tanzania, harufu ya kupewa heshima ya kuwa na sanamu lake inakuja halafu inakataa, kwa nini Tusiweke ya Samatta?”

 

Mchomvu pia alimzungumzia Harmonize na AliKiba:
“Hamonize amejipanga na menejimenti yake, AliKiba ni mtu smart, ana ngoma zake nzuri sana na nafikiri yule jamaa sio wa kutoa ngoma leo kesho, ngoma zake ziko pale zina stay.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad