Mchungaji Aamuru Waumini Wake Kubusiana Wapate Upako



- Pasta mmoja aliwamuru waumini kubusiana wakati wa ibada

- Katika picha, waumini hao wanaonekana kufuata agizo la pasta huku kila mmoja akimbusu mwenzake

- Kanisa hilo la Hope Restoration Ministries, linasemakana kuwa kanisa maarufu sana nchini Afrika Kusini

Je ni sawa kwa waumini kubusiana ndani ya kanisa huku ibada ikiendelea?

Nchini Afrika Kusini, kanisa moja limezua gumzo kwenye mtandao jamii baada ya waumini kunaswa wakibusiana wakati wa ibada.

Kanisa
Pasta mmoja aliwamuru waumini kubusiana wakati wa ibada.Picha:Photo: Hope Restoration Ministries.
Pasta wa Hope Restoration Ministry aliamuru kondoo wake kubusiana wakati wa ibada.

Katika picha ambayo imesambaa kwenye mtandao jamii, waumini hao walifuata agizo la mhubiri wao huku kila mmoja akinaswa akimbusu mwenzake.

Mhubiri huyo anaripotiwa kuamuru kusema "Chukua jirani yako na mbusu".

Haijabainika wazi sababu za pasta huyo kutoa amri hiyo na ni mstari upi wa bibilia alikuwa anautumia.

Pasta aamuru waumini kubusiana kanisani wakati wa ibada
Katika picha, waumini hao wanaonekana kufuata agizo la pasta huku kila mmoja akimbusu mwenzake.
Kanisa la Hope Restoration Ministry linasemekana kuwa miongoni mwa makanisa kubwa nchini Afrika Kusini lenye washirika wengi.

Inaripotiwa kuwa picha hizo zilipigwa wakati wa siku ya Valentines Dei ili kupamba ndoa.

Haya ni kulingana na ujumbe kwenye Twitter kutoka kwa mkuu wa kanisa hilo Rev. Chris Mathebula.

Wakati huo huo, sio mara ya kwanza kwa tukio sawia na hilo kushuhudiwa kanisani.

Pasta maarufu wa Kenya, James Ng’ang’a, alikaripiwa na mwanadada mmoja aliyejitambulisha kama Shetani kutoka Gatundu.

Pasta huyo bila uwoga alianza kukabiliana naye ambapo mwanamke alianza kumuonyesha ishara za kishetani.

Kioja hicho kanisani kilizua mjadala mtandoani pamoja na mavazi ya mwanadada huyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad