KUPITIA ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, amesema ameitwa jijini Dodoma kwenye kikao cha Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema amepata barua ya kuitwa jana na atahudhuria bila kukosa au kuchelewa kikao hicho kitakachofanyika Februari 6, mwaka huu saa 3 asubuhi kwenye Jengo la White House.
Mwaka jana kulisambaa sauti zinazohusishwa kuwa ni za Membe na wengine waliowahi kuwa viongozi wa CCM wakizungumzia kuhusu mpasuko ndani ya chama hicho na pia kusikika wakilaumu uongozi ulipo sasa.
“Hatimaye, jana jioni nimepokea barua ya kuitwa kwenye kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu Jijini Dodoma. Kikao kitafanyika tarehe 6/02/2020 saa 3 Asubuhi kwenye jengo la White House. Nitahudhuria bila kukosa na bila kuchelewa! Stay tuned!”