Mfanyakazi wa Kenya Air Ways Aliyesambaza Video ya Ndege ya China Ikitua Kenya Afukuzwa Kazi..Aofia Maisha yake



Afisa wa ulinzi ambaye alisimamishwa kazi baada ya kusambaza kanda iliyoonesha ndege ya Shirika la China Southern Airlines ikitua katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege (JKIA) anaishi kwa hofu.

Gire Ali aliachishwa kazi Alhamisi, Februari 27 na meneja wa ajira wa shirika hilo Evelyne Munyoko kwa madai ya utovu wa nidhamu alisema amekuwa akipokea simu kutoka kwa watu asiowafahamu.

Mfanyikazi wa KQ aliyesambaza video ya ndege ya Uchina ikitua JKIA alipigwa kalamu Alhamisi,
"Watu wengi wamekuwa wakinipigia simu, lakini nahofia huenda baadhi yao wanapeleleza kule niliko. Nimegoma kupokea simu kwa kuwa sijui wanaonipigia ni akina nani kwani huenda wana nia mbaya," aliiambia k24 Ijumaa, Februari 28.

Baada ya video hiyo kupenyeza mitandaoni, Ali alisema aliagizwa kufika katika afisi ya bosi wake ambapo alihojiwa kwa zaidi ya saa sita kabla ya kuambiwa kuviregesha vifaa vyake vya kazi.

Kulingana na Idara ya kuwaajiri wafanyikazi wa shirika hilo, uamuzi wa kumuachisha kazi kwa muda Ali uliafikiwa kwa minajili ya kuendeleza uchunguzi zaidi kuhusiana na jambo hilo.

Mhudumu wa Shirika la ndege la China Southern Airlines ambalo lilisitisha safari zake za Nairobi kwa muda. Picha: China Southern Airlines.

"Umachishwa kazi kwa muda baada ya kuhusika katika usambazwaji wa video iliyoonesha ndege za Shirika la China Southern ikiwasili nchini JKIA kuanzia Februari 27," Munyoki alisema.

Gire ambaye anahofia kuwa huenda akapoteza kazi yake alisema kwamba aliagizwa kufika katika afisi za upelelezi na vile vile kwa meneja wake kila anapohitajika.

Ndege hiyo ya Uchina iliwaleta abiria 239 nchini licha ya kuwepo kwa hofu kuhusu virusi vya Corona nchini humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad