Mgonjwa wa Corona Ujerumani yuko mahututi



Wizara ya afya ya jimbo la North Rhine Wesphalia nchini Ujerumani imesema hii leo kwamba mtu alliyeambukizwa virusi vya Corona yuko katika hali mbaya na amepelekwa kwenye hospitali ya madaktari bingwa iliyoko kwenye mji wa Duesseldorf.

 Kulingana na wizara hiyo, mtu huyo anayetokea mji wa Erkelenz karibu na mpaka wa Uholanzi kwa mara ya kwanza alilazwa siku ya Jumatatu akiwa na homa kali ya mapafu. Lakini baadae aligundulika kuambukizwa virusi hivyo na kutengwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kupelekwa Duesseldorf.

Mke wake pia ametengwa kufuatia wasiwasi kwamba ameambukizwa virusi hivyo baada ya kuanza kuonyesha dalili. Tayari watu 80,000 wameambukizwa virusi hivyo kote duniani, huku Ujerumani ikiwa ni wagonjwa 17, idadi hii ikiwa ni kulingana na shirika la afya ulimwenguni, WHO.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad