Mhadhiri akutwa amekufa na kamba shingoni



Profesa Gil Gil Ogutu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, amekutwa amekufa nyumbani kwake katika kijiji cha Wambasa kilichopo Bondo, Kaunti ya Siaya.

Mkuu wa eneo hilo, Gordon Opundo alisema mwili wa Profesa Ogutu ulipatikana ukiwa umeninginia kwenye dirisha la chumba chake huku ukiwa na kamba iliyofungwa shingoni

Taarifa zinasema mwili wa Mhadhiri huyo uligunduliwa na mfanyakazi wake siku ya Jumapili muda wa saa tatu asubuhi

Aidha, taarifa zinadai kuwa Profesa huyo siku ya Ijumaa alikwenda nyumbani na mke wake wa pili na wawili hao walikuwa pamoja hadi Jumamosi jioni wakati anaripotiwa kuwa aliondoka kwenda Kisumu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad