Miaka 9 Katika Ndoa - Simuelewi Mume Wangu Ajanigusa Miezi Sita Sasa Naomba Ushauri


Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 33 mume wangu ana umri wa miaka 41. Sote ni wasomi na wafanyakazi. Tumefunga ndoa miaka tisa iliyopita tuna mtoto mmoja ana umri wa miaka 7.Wakati tunafunga ndoa wote tulikua mabikra. Mimi nilikua sijawahi kuwa na mpenzi na mume wangu akuwahi kua na mpenzi..

Tulianza kushiriki tendo la ndoa siku ile tulipofunga ndoa. Kwa kweli kwa ujumla maisha yetu ya ndoa ni ya furaha kwa mambo yote lakini sio ya kiunyumba.

Mimi na mume wangu atujawahi kuwa mbali kikazi. Maisha yote hadi leo tuko Dar es salaam pamoja. Tulipofunga ndoa miaka ya mwanzoni tulikua tunaweza kukutana kimwili hata mara tatu kwa mwezi, miaka ilivyokua inazidi kwenda ikawa kukutana kimwili inakua mara moja kila baada ya miezi miwili na tukikutana ni bao moja tu.

Sasa hali imezidi kua mbaya kwani sasa imepita miezi sita tunalala kitanda kimoja mume wangu ajanigusa, hali hii inanisononesha kwani natamani mtoto wa pili. Kwakweli atuna ugomvi wowote. Mimi na mume wangu wote ni wacha Mungu.

Mume wangu ni mchapakazi sana tukitoka kazini tuko wote na sio mtu anaependa kwenda kutembea bila familia. Jumamosi na Jumapili mara nyingi tunatoka out tukirudi home akuna kinachoendelea, anageuka ukutani analala kama mtoto hadi asubuhi, wala hata anigusi nikimsogelea hata ashtuki.

Na asubuhi tukiamka tunaenda ofisini na akifika ofisini lazima anitumie message, mke wangu nakupenda sana. Simuelewi na nashindwa kumuuliza maana mimi kama mwanamke naona aibu.

Kwakweli mawazo ya kutoka nje ayapo kabisa kichwani mwangu maana simjui mwanaume mwingine zaidi yake pia namuogopa Mungu siwezi kucheat.Ila kwa hali ilipofikia naona bora nitengane nae niishi maisha yangu maana bila unyumba amna maana ya ndoa na nataka sana mtoto.

Wadau naomba ushauri je hii ni kawaida, nifanyeje.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah mwoneni Mtaalam wa mambo ya uzazi na magonjwa yatokanayo na via vya uzazi unakuta mtu ana tatizo kusema anaona aibu au anahisi utamkimbia vitu kama hivyo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad