Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema miili ya watu 20 waliofariki kwenye kongamano la Mtume na Nabii Mwamposa, itaagwa kesho Februari 3, 2020, kwenye viwanja vya Majengo mjini Moshi. Amesema hadi sasa tayari miili 16 imeshatambuliwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro amewataka Watanzania kuwa makini kwani kinyume na hapo itakuwa shida sana na kuongeza iko haja kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa kuanza kuyafuatilia makanisa yote nchini na hasa makanisa madogo madogo ambayo sasa yamekuwepo kila mahali.
"Sio kila padri, mchungaji basi anataka kuwachunga kondoo wake waende kuuona ufalme wa Mungu, wengine wanahangaika na utafutaji tu wa maisha.Sio kwamba nahukumu lakini kuna mambo ya kujifunza,"amesema
Kuhusu Polisi iwapo walikuwepo kwenye kongamano hilo la Mwamposa, IGP Sirro amesema ameshatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimajaro kufuatilia na iwapo walikuwepo polisi lazima waulizwe imekuaje hadi watu wakapoteza maisha na wao wakiwepo, kwani sheria lazima ichukue mkondo wake.
Poleni Wafiwa.
ReplyDeleteNaomba Serikali na Viongozi wa makanisa yote nchini na wana taaluma
na baraza la Lugha yetu fasihi ya Kiswahili Uhalali wa kutumia s
Siafa ya Kujiita NABII au MTUME.!!
Na sifa ambatanishi zilizotukuka.
TUJUE NA KUPIGA MARUFUKU UTAPELI
NA UTUMIAJI HARAMU KUJIPATIA KIPATO
WASICHO STAHILI.
NABII..??? MTUME..???
JAMANI MNPOTOSHA LUGHA YETU.
HAMUITENDEI HAKI.
Poleni Wafiwa.
ReplyDeleteNaomba Serikali na Viongozi wa makanisa yote nchini na wana taaluma
na baraza la Lugha yetu fasihi ya Kiswahili Uhalali wa kutumia s
Siafa ya Kujiita NABII au MTUME.!!
Na sifa ambatanishi zilizotukuka.
TUJUE NA KUPIGA MARUFUKU UTAPELI
NA UTUMIAJI HARAMU KUJIPATIA KIPATO
WASICHO STAHILI.
NABII..??? MTUME..???
JAMANI MNPOTOSHA LUGHA YETU.
HAMUITENDEI HAKI.
Binafsi i feel sorry ila ujinga wao ndio umewapeleka kwa nabii fake. Wacha wajifie, ndio nchi pia itajisafisha maana wajinga wamekuwa wengi.
ReplyDelete