Mkapa Aeleza Alivyowagomea Waliotaka Abadili Ukomo wa Urais
0
February 24, 2020
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amefichua jinsi baadhi ya wazee wa Zanzibar walivyomtembelea kumshawishi aruhusu mabadiliko ya katiba kumwezesha aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo kuongoza kwa awamu tatu badala ya mbili za kikatiba.
Akizungumza jijini Mwanza juzi wakati wa hafla ya kutambulisha kitabu chake, Mkapa alisema suala hilo lilikuwa kiunzi ambacho kilikaribia kumuingiza kwenye mtikisiko kiuongozi.
“Nilikaribia kupata mtikisiko lakini nilifanikiwa kuruka kiunzi hicho ingawa ilikuwa kazi nzito kweli. Tulizungumza kwa makini na hatimaye tulielewana; na katiba ya Zanzibar ikabaki na vipindi viwili vya miaka mitano kama ilivyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” alisema
Alisema kufanikiwa kuruka kiunzi hicho ni miongoni mwa mambo anayojivunia na kuona ufahari kwa sababu aliweza kulinda Katiba ya Zanzibar na ile ya Muungano hadi alipokabidhi kijiti cha uongozi kwa Rais Jakaya Kikwete.
Tags