Mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane alipandishwa kizimbana kwa Kumuua Mke wa Kwanza wa Waziri Huyo




Mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane alipandishwa kizimbana jana kwa tuhuma za kumuua mke wa kwanza wa kiongozi huyo siku mbili kabla ya mumewe hajababidhiwa ofisi mwaka 2017.

Mashtaka yaliyowasilishwa mahakamani mjini Mbabane yamesema Maesaiah alimpiga risasi kwa nia ya kuua Lipolelo Thabane na kumjeruhi kwa bunduki. Waraka wa mashtaka hayo haukutoa maelezo zaidi.

Mwezi uliopita polisi ya Lesotho ilitoa kibali cha kutiwa nguvuni mke wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Maesaiah baada ya kukataa kwenda kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo na baadaye akatoweka kabisa.

Kabla ya Lipolelo kuuawa hapo maka 2017, mke huyo wa zamani wa Waziri Mkuu wa Lesotho na mumuwe walikuwa katika mchakato wa talaka. Ni wakati huo ndipo aliposhambuliwa na kupigwa risasi na mtu asiyejulikana karibu na nyumba yake mjini Maseru, siku mbili kabla ya mumewe kuidhinishwa kama Waziri Mkuu. Wakati huo iliaminika kuwa tukio hilo lilikuwa mauaji ya kisiasa.

Maesaiah na Waziri Mkuu wa sasa wa Lesotho, Thabane Lipolelo walioana miezi miwili baadaye.

Kesi hii ya mauaji yaliyodaiwa kufanywa na mke mdogo wa Waziri Mkuu wa Lesotho dhidi ya mke wake wa kwanza, imechochea upinzani na maandamano makubwa ya wananchi katika nchi hiyo ya milimani inayozungukwa na Afrika Kusini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad