Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet ((54) raia wa Uturuki amehukumiwa kulipa faini ya USD milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukiri shtaka la kushindwa kutoa tamko la fedha USD 84,850 alizokutwa akizisafirisha.
Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa fedha hizo zote kuwa mali ya serikali.
Mehmet ambaye nchini Tanzania anaishi Ilala jijini Dar es salaam amesomewa hukumu yake na Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kufikishwa mahakamani leo Februari 27 ma kusomewa shtaka moja la kushindwa kuzitolea taarifa fedha alizokutwa kusafiri nazo.
Mapema akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mkuu Shadrack Kimaro amedai kuwa Februari 13, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal III jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa anaondoka nchini kwenda Instabul Uturuki alikutwa na USD 84,850 ambazo hakuwa amezitolea taarifa kwa Idara ya Forodha.
Mapema akisoma maelezo ya awali kabla ya kusomewa adhabu wakili Kimaro alidai mshtakiwa Mehmet ni raia wa Uturuki na ameajiliwa na kampuni ya Yapi Merkezi ambayo inashughulika na ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge hapa nchini Tanzania.
Imedaiwa siku hiyo alikuwa akisafiri kuelekea Instabul Uturuki kwa kutumia ndege ya Turkish namba TK 0604 huku akiwa amebeba mabegi. Akiwa amefuata taratibu zote za uwanja wa ndege akiwa anaelekea kupanda ndege alikutwa na Ofisa wa usalama akiwa na kiasi hicho cha fedha ambazo hakuwa amezitolea taarifa.
Aidha imedaiwa fedha hizo zimehifadhiwa NMB banki kwenye kitendo cha intelejensia.
Mahakama pia imeamuru mshtakiwa kurudishiwa pasi yake ya kusafiria na tiketi yake ya ndege.
Akamatwe na Dola elfu 85.
ReplyDeleteAlipeDolla Miliono tena siyo Ilioni Moja ia M100.
Mbona haiingii kichwani..?? mnao tuhabarisha mmechemshaau mimi sielewi??..!!!!
Halafu pesa yake TUMEEI TAIFISHA. SI ADHABU TOSHA.
HALAFU HAWA SI WANATUJENGEA SGR. NA UHUSIANO WETU KABUDI SI UTALEGA.
Tume mchunguza, uhalali wa yeye kuwa nakiasi hicho keshi na lengo la kuzishika ni lipi, je alizitoa benki na chanzo kilikuwa malipo gani.
DeleteJE UONGOZI WAKE WANAJUA KWAMBA ALIKUWA ANAZO HIZI PESA NA ANAONDOKA NA HIYO SIKU??