Mkuu wa Mkoa 'Ataja' Dawa Mpya ya Nguvu za kiume



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema hakuna dawa nyingine ya nguvu za kiume zaidi ya kutafuta pesa ambayo itamuwezesha mtu kupata kitu chochote anachokihitaji.

Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza mkoani Mbeya wilayani Rungwe, wakati akizungumzia juu ya mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha makundi maalum.

Chalamila amesema kuwa "usijisumbue ukaenda kwenye kibao kimendikwa huku zinapatikana nguvu za kiume, ni waongo, nguvu za kiume ni fedha wewe tafuta mshiko tu halafu kaa kimya kama Bubu hata mwanamke utapata, lakini unaondoka na mikwara hauna chochote mfukoni hata ukienda Hospitali utaambiwa una upungufu wa nguvu za kiume kwa 406%"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad