Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wafanyabiashara wadogo (machinga)kuacha kufanyabiashara kwenye maeneo ya mahakama kwa kuwa wanazuiya njia wananchi wanaenda mahakamani hapo kwa shughuli za mahakama.
Na kuagiza wanaofanyabiashara maeneo hayo kuona umuhimu wa kuyaachia Mara
moja ili kuifanya mahakama kufanyakazi zake kwa utulivu na kuondoa adha kwa
wananchi wenzao kwa kuwa hakuna mhimili usio na faida yote ipo kwa mujibu
wa sheria hivyo tufanyekazi kwa kuheshimu sheria kwa kuwa wote tupo kwa
ajili ya kuwatumikia wananchi.
Kwa muktadha huo akatoa angalizo kwa viongozi wa wamachinga wanaofanya
biashara kwenye maeneo ya mahakama kukaa pamoja na viongozi wa mahakama na
mkoa kuainisha maeneo ya mahakama ili kuona namna nzuri ya kuondoka katika
maeneo hayo ya mahakama kwa wafanyabiashara hao bila kusukumana.
Agizo hilo amelitoa kwenye siku ya sheria na mwaka wa mahakama iliofanyika
jijini Arusha ambapo alisema kuwa atakaa na watendaji wa mahakama viongozi
wa wamachinga kuona namna nzuri ya kupanga ili kuwezesha shughuli za
mahakama kufanyika bila bughudha.
Kwa mujibu wa Gambo aliwataka Mahakimu wote kutenda kazi kwa kufuata kanuni
tusicheleweshe Wala kuahirisha kesi za wananchi kwani zinaongeza gharama
kwa kutojua mwananchi ametoka umbali gani.
Alieleza kuwa Elimu ya sheria na adabu za mahakama zinatakiwa kutolewa kwa
wananchi ili kuondoa changamoto kwa wananchi kupata adha ambazo zinaepukika
kwa kutumia muda mfupi wa kushughulikia mashauri mapema na kuangalia Jambo
lenyewe ili kuongeza utoaji haki.
“Tutumie utu na kujali dhamana tulizopewa kwa lengo la kutumia madaraka
yetu vizuri,angalieni changamoto ya utoaji wa nakala za hukumu ili kuondoa
kero na adha kwa wananchi wetu, tuangalie jinsi ya kuondoa vitendo vya
kihalifu kwa kutumia sheria zilizopo kwa kuwa wakweli,pia kumekuwa na
changamoto za kubambikiwa kesi na ucheleweshaji wa mashtaka nendeni
mkaliangalie hayo”alisema Gambo
Alisema kuwa haki inayocheleweshwa iangaliwe ili kuondoa kero kwa kutumia
muda na kutocheleweshwa kwa kesi na hivyo wananchi kutopata haki yao kwa
wakati kwa kila moja kutimiza wajibu wake katika mashauri yanayoletwa
mahakamani,hivyo viongozi tuheshimu mihimili iliyopo ili kuwafanya wananchi
kuheshimu sheria na mahakama.
Kwa Upande wake Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha Mosses Mzuna
alisema kuwa watumishi wajipambanuwe kwa lengo la kutoa haki kwa wakati
kuendana na dhumuni kubwa la sheria ni kuhamasisha mahusiano ya biashara.
Alisema kuwa uwekezaji wa kibiashara ni kutega fedha au uchumi ndio maana
mahakama ikaona umuhimu kuiweka katika kauli mbiu yake ya mwaka huu ili
uwekezaji na mazingira wezeshi iwe sehemu ya utoaji haki na sehemu ya
mahakama.
“Sheria zetu hazipo mbinguni zipo duniani hivyo mahakama iende na kuangalia
masuala ya kiuchumi ili ziweze kuendelea, kwa kuenda sambamba na utoaji
haki kwa kuharakisha migogoro ya kibiashara kwa lengo la kuvutia wawekeza
ambao wataweka mitaji mikubwa kwa kuwa watakuwa na Imani na mahakama
zetu”alieleza Jaji Mzuna akisoma nukuu ya Rais mstaafu Mkapa
Alisema mahakama kama hazitachelewesha mashauri na kutoa haki kwa wakati
hakika ongezeko la Masha Bora jamii inayopenda kujifunza zaidi amani na
utulivu nasi kama mahakama hatuwezi kujitenga kwenye sera hiyo kwa
kushirikiana na wadau.