Msafara wa Profesa Lipumba Wapata Ajali


Msafara wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, umepata ajali ukishuka milima ya Ndororo mkoani Morogoro baada ya gari yake moja kufeli breki na kuingia ndani ya mfereji.


Katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Februari 24, 2020, hakuna mtu aliyeumia ambapo Profesa Lipumba pamoja na vijana wake wanaendelea na harakati zao.

Mbali na ajali hiyo katika ziara yake amekwama barabarani kufuatia ubovu wa miundombinu ya barabara ya kuelekea Kijiji cha Iputi kata ya Mbuga wilayani Ulanga mkoani humo na kulazimika mwenyewe kuingia mzigoni.

Katika ziara yake ya kuimarisha chama amegawa zaidi ya kadi 600, katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Morogoro, huku asilimia kubwa ya wananchi wakirudisha kadi za CCM na CHADEMA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad