Baada ya uvumi wa kuvunjika kwa ndoa yao, hatimaye Ne-Yo amethibitisha kupeana talaka na mke wake, Crystal Smith.
Kwenye mahojiano na Podcast ya Private Talk wiki iliyopita, Ne-yo alisema "Ilianza chini chini lakini ikawa imefika kwa watu, Ni kweli Mimi na mke wangu tumefikia kupeana talaka." alisema Ne-Yo ambaye walifunga Ndoa mwaka 2016 na kupata watoto wawili.
Aliendelea kusema "Sio kitu cha kusikitisha, ni kitu cha kutambua tu, kufupisha stori, sitakuja kumuongelea vibaya. Sio mtu wa hivyo. Ni mwanamke mzuri sana. Ni mama wa watoto wangu wawili na atabaki kuwa hivyo." alimaliza Ne-Yo.