Msanii wa maarufu wa nyimbo za Injili Rwanda anayedaiwa kujiua anazikwa leo




Msanii maarufu wa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo ambaye aliripotiwa kujiua katika mahabusu ya polisi nchini Rwanda anazikwa leo nchini Rwanda.

Mamia ya watu wamejitokeza kuusindikiza mwili wa Bw. Kizito Mihigo, akiwemo Bi Diane Rwigara, mwanasiasa wa upinzani na mfanyabiashara mjini Kigali

Bw. Alifariki siku tatu baaada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Burundi, polisi wakimtuhumu kwa jaribio la kutaka kutoroka nchi na kujiunga na la waasi linalopigana dhidi ya serikali ya Rwanda.

Kifo cha Mihigo kiliibua hisia tofauti miongoni mwa wanyarwanda wanaoishi ndani na nje ya nchi huku wakitaka uchunguzi ufanyike kujua kilichosababisha kifo chake.

Kizito mihigo alikua maarufu sana kwa nyimbo zake za injili zilizoikonga mioyo ya Wanyarwanda na Warundi wa ndani na nje ya nchi:

Mashirika ya kibinadamu pia yalitilia shaka kifo chake na kutaka uchunguzi huru ufanyike kuhusiana na kifo hicho.

Hata hivyo Rwanda imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya kutaka uchunguzi huru kufanywa kuhusu kifo cha msanii maarufu wa muziki wa kiinjili Kizito Mihigo, ambaye alipatikana akiwa amefariki katika kituo cha polisi Jumatatu asubuhi.

Msemaji wa shirika la upelelezi la Rwanda, Marie Michelle Umuhoza, aliimbia BBC kwamba "Rwanda ni nchi huru inayojitawala na ambayo ina uwezo wa kuchunguza wa kitu chochote".

Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights Watch, Amnesty International na Commonwealth Human Rights Initiative yamekuwa yakishinikiza kufanyika kwa uchunguzi huru wa kubaini mazingira yaliyosababisha kifo cha mwanamuziki huyo aliyekuwa na miaka 38- amabaye alizoa umaarufu kutokana na ujumbe wake wa amani na maridhiano.

Afisa wa Human Rights Watch aliiambia BBC kwamba uchunguzi huru utaangalia kamera za siri katika eneo ambalo msanii huyo alikuwa anazuiliwa.

Lakini Umuhoza alisema Rwanda tayari inafanya uchunguzi kuhusu kifo chake.

"Sioni haja ya kufanyika kwa uchunguzi huru, katika nchi huru", alisema, bili kuangazia uchunguzi wao utakamilika lini.

Wanaharakati na marafiki wa Mihigo walisema kwamba mwanamuziki huyo hakutaka kujiunga na kundi la waasi nchini Burundi kama ilivyotajwa na maafisa wa usalama wa Rwanda na kwamba alitaka kwenda Ubelgiji ambapo alikuwa akiishi.

Pia wanaamini kwamba hakujiua katika kituo cha polisi alipokuwa anazuiliwa na kwamba huenda aliuawa.

Muziki wa Kizito ndio chanzo cha matatizo yaliomkumba. Katika wimbo mmoja alipendekeza kwamba kila mtu aliyeuawa katika mauaji ya kimbari ya 1994 anapaswa kukumbukwa awe Mtutsi ama Mhutu.

Wanasema kwamba mamlaka imeliona hilo kama changamoto ya wazi dhidi yake na kwamba mauaji hayo yalitekelezwa na Watutsi.

Wakosoaji wa serikali wanaamini kwamba kutokana na hilo Kizito alilengwa.

Mwanamuziki huyo alikuwa ameanza kuchunguzwa kuhusiana na madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkamata.

Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.

Kumekuwa na hisia mseto katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha ghafla cha msanii huyo wa muziki wa injili huku baadhi ya watu wakitaka majibu kutoka kwa serikali.

Kizito, aliyekuwa na miaka 38 alipata umaarufu kutokana na nyiimbo zake kama vile 'Inuma' unaomaanisha njiwa na 'Igisobanuri cy'urupfu' ambao unaelezea kifo ni nini.

Lakini baadhi ya watu wanaamini wimbo wake Igisobanuro cy'urupfu, ambayo tafsiri yake ni "maana ya kifo", aliyotoa mwaka 2014 siku kadhaa kabla ya kumbukumbu ya 20 ya mauaji ya kimbara ya Rwanda, ndio iliyomtia mashakani- kwa kugusia kile kinachodaiwa kuwa uhalifu uliofanywa na chama tawala cha Rwanda Patriotic Front.

Mihigo, ambaye alikuwa aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 mwaka 2015 kwa kupanda njama ya kupindua serikali, na kuachiliwa baadaye kwa msamaha wa rais Septemba 15 mwaka 2018 pamoja na wafungwa wengine zaidi ya 2,000.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad