Mshauri wa Rais Trump Akutwa na Hatia, Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Mitatu



Roger Stone,  aliyekuwa mshauri wa Rais wa Marekani, Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi ambaye jina lake lilitajwa wakati wa kesi ya Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 3 na miezi 4.

Uamuzi kuhisiana na kesi zilizokuwa zikimbali Stone umetolewa katika mahakama jijini Washington. Miongoni mwa tuhuma saba zilizokuwa zikimkabili ni pamoja na “kulidaganya bunge” na “kuzuia haki isitendeke”.

Hakimu Amy Berman Jackson, alitoa hukumu ya kifungo cha miaka 3 na miezi 4 kwa Stone.

Stone alikamatwa mwaka jana mwezi Januari, katika tuhuma ambazo zilikuwa zikihusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016, uchunguzi wa tuhuma hizo uliendeshwa na mjumbe maalum, mwanasheria msomi  Robert Mueller.


SOMA HABARI HIZI KUPITIA APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD > HAPA

Katika hati ya mashitaka Stone alihusishwa na kuvuja kwa ujumbe wa barua pepe wa aliekuwa msimamizi mkuu wa kampeni wa mshindani wa Rais Trump katika uchaguzi mkuu wa Rais Bi Hillary Clinton. Ujumbe huo ulifika katika computa za maharamia wa mtandao wa kirusi na kishwa kusambazwa katika kurasa za mtandao za Wikileaks.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad