Mtu mfupi zaidi kutoka Tanzania aingia kwenye rekodi ya Dunia


Masoud Hussein kutoka mkoani Arusha, ameingia kwenye rekodi ya Dunia kwa kuwa mtu mfupi zaidi kupanda Mlima Kilimanjaro, katika kitabu cha rekodi maarufu zaidi duniani kijulikanacho kama Guinness World Records.

Masoud Juma alikuwa mgeni wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla, ambaye amesema ametumia muda wake wa kumpa mchango wa senti, mawazo, mbinu, na siri ya mafanikio ili afanikishe misheni yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,  Hamisi Kigwangalla ameeleza kuwa,

"Huyu ndugu niliyenaye hapa ni mgeni wangu bungeni leo, anaitwa Masoud Juma Hussein, wa Arusha ameingia kwenye "quest" ya kuweka rekodi ya kuwa mtu mfupi zaidi duniani kupanda Mlima Kilimanjaro, ameisajili azma hii kwenye kitabu cha rekodi maarufu zaidi duniani kijulikanacho kama Guinness World Records, tumuombee kheri" ameandika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad