Mtu mmoja afa kwa virusi vya Corona Italia



Mwanaume mmoja wa Italia aliyekuwa ameathirika na virusi vya Corona amefariki dunia na hivyo kifo hicho kuwa cha kwanza kutokea barani Ulaya.

Waziri wa Afya wa Italia, Roberto Speranza amesema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 78, alifariki jana kwenye hospitali ya mji wa Padua, alilokuwa amelazwa kwa siku 10.

Mwanaume huyo alikuwa miongoni mwa watu wawili waliokutwa na virusi vya Corona vinavyojulikana kama COVID-19 katika mkoa wa Veneto.

Maafisa wa Italia wameamuru kufungwa kwa shule, majengo ya umma pamoja na migahawa kwenye miji 10 ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo, Korea Kusini leo imeripoti visa vipya 142 vya Corona na kuifanya idadi jumla ya walioambukizwa nchini humo kufikia 346.

Idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya Corona nchini China imefikia 2,345 baada ya vifo 109 kuongezeka jana na walioambukizwa ni 76,000.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad