Mwamposa Atafutwa na Polisi Kwa Mahojiano...Ajulikani Alipo



Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha Polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea Mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Salum Hamduni amesema Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu na kwa sasa Mchungaji huyo anashikiliwa na Polisi pamoja na watu wengine 6

Amesema, baada ya hilo tukio wamemtafuta sana Boniface Mwamposa maarufu kama "Bulldozer" bila mafanikio na hivyo kumtaka ajisalimishe Polisi mwenyewe

Kamanda Hamduni alifafanua kuwa, idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne na watu wazima 16
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad