Mkenya mmoja aliyetangaza hadharani kupitia mitandaa ya kijamii kuwa ni shoga, amepatikana akiwa ameuawa nchini Marekani
Mwili wa Paul Lukas ulipatikana Jumatano, Februari 12 baada ya kuripotiwa kutoweka kwa siku tatu.
Mkenya aliyetangaza hadharani kuwa shoga apatikana ameuawa Marekani
Mkenya aliyetangaza hadharani kuwa shoga apatikana ameuawa Marekani
Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa TUKO.co.ke, Lukas ambaye alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha East Africa School of Media Studies alikuwa akifanya kazi katika shirika la ndege la Alaska.
" Ninataka kila mtu ajue kwamba mimi ni shoga, nimechoka na kuishi maisha ya uongo," Lukas alisema.
Mkenya aliyetangaza hadharani kuwa shoga apatikana ameuawa Marekani
Mwili wa Paul Lukas ulipatikana Jumatano, Februari 12 baada ya kuripotiwa kutoweka kwa siku tatu.
Marehemu anasemekana kuwa katika hali njema kabla ya kifo chake na wanaomjua wanashangaa ni nini kilisababisha kifo chake.
Taarifa zingine ziliarifu kuwa huenda marehemu alipigwa risasi na watu wasiojulikana.
Uchunguzi zaidi unatarajiwa kufanywa ili kubaini chanzo cha kifo chake.