Mzee wa Sumbawanga Aeleza Anavyotengeneza Radi.....
0
February 27, 2020
Mzee Fabiani mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 anayeishi Sumbawanga mkoani Rukwa ambaye ni maarufu sana kutokana na uwezo wake wa kutengeneza radi kwaajili ya kujikinga na mabaya pamoja na kutoa tiba mbalimbali za asili kwa watu wenye magonjwa au matatizo yao mengine amefunguka jinsi anavyotengeneza radi na kuituma.
Mzee Fabiani amefunguka jinsi anavyotoa huduma zake kwa watu mbalimbali ikiwemo watu wa kutoka mataifa tofauti kama Congo, Kenya na hata Afrika Kusini ambao mara nyingi wamekuwa wakienda mpaka Sumbawanga kutafuta tiba yake hiyo.
Mzee Fabiani amesema ni kweli ana uwezo wa kutengeneza radi na kuituma kwa mtu au sehemu yoyote ile ambapo kuna mbaya wa mtu na kupelekea madhara kwa mtu huyo hata kama ni mchana kweupe pasipo na mvua.
Mzee Fabiani amesema kuwa ila hupenda kutuma radi hiyo Vipindi au nyakati za mvua ili kuepuka taharuki na mtafaruku katika jamii ambapo huona kuwa ni kawaida radi kupiga wakati wa mvua.
Mzee Fabiani amesema uwezo huo amerithi kutoka kwa wazee wake ambao nao pia walilithi kutoka kwa mababu zao.
#RADI NI NINI?
(WHAT IS THUNDERSTORMS?)FAHAMU KUHUSU MADHARA YA RADI NA NAMNA YA KUJIKINGA NA RADI KIPINDI HIKI CHA MVUA .
•Katika vipindi vya Mvua ni kawaida katika baadhi ya sehemu ya dunia watu kuona mwanga mkali wa ajabu unaoambatana na sauti kubwa ya muungurumo (sauti yenye mitetemo) au ya kawaida ikisikika na kuonekana angani. Mwanga huo angani na sauti za muungurumo hufahamika kama RADI.
•Radi Huwatisha sana watu na wanyama kwani katika maeneo mbalimbali Radi husababisha madhara kama vile kujeruhi watu na wanyama, kuua watu na wanayama, vile vile kuharibu mali mbalimbali za watu kwa kuzichoma, mali kama vile vifaa vya umeme, Miti, nyumba, miundombinu mbalimbali ,nakadhalika huaribiwa vibaya na kuwaacha watu wakilia kwa hasara kubwa.
•Kitendo cha watu na wanyama kuogopa sana RADI kitaalamu hufahamika kama ASTRAPHOBIA
1. RADI NI NINI NA HUTOKEAJE?
•Kwanza jambo la muhimu la kulijua hapa ni kwamba katika mawingu kuna UMEME (electric charge) ambao huzaliwa juu katika mawingu.
•Hivyo jibu rahisi pale unapoulizwa Radi ni nini, jibu lake ni "RADI ni UMEME"
•Radi hutokea katika mawingu yanayofahamika kitaalamu kama CUMULONIMBUS CLOUD. Mawingu haya hutengenezwa kutokana na mvuke wa maji kutoka katika vyazo vya maji kama vile bahari, maziwa na mito, ambapo baada ya maji kupata joto hubadirika kua mvuke (Water Evaporation) na kusafirishwa angani mwishoni hugeuzwa kua mawingu.
JINSI UMEME UNAVYOZALISHWA KATIKA MAWINGU
•Upepo mkali unaovuma katika mtindo wa duara juu ya mawingu huyabeba matone ya maji kutoka chini ya mawingu na kuyapeleka juu kabisa ya mawingu ambako kuna hali ya baridi sana, hivyo matone hayo ya maji hugandishwa na kua BARAFU. Vivyo hivyo upepo pamoja na mvutano wa dunia (gravitational force) huvibeba vipande hivyo vya barafu kutoka sehemu ya juu kabisa ya mawingu na kuvipeleka chini ya mawingu.
•Vipande vya barafu vinavyosukumwa kwenda chini kutoka juu kabisa ya mawingu (DOWNDRAFTS) hukutana na kusuguana na matone ya maji yanayosukumwa kutoka sehemu ya chini ya mawingu kwenda juu (UPDRAFTS), kitendo cha MSUGUANO wa vitu hivi viwili vinavyokutana njiani kimoja kikipelekwa juu kingine kikipelekwa chini, huzalisha CHAJI za UMEME ambazo ni Chaji Hasi (-) na Chaji Chanya (+) au Positive charge (+) na Negative charge (-)
•Chaji hizi NEGATIVE CHARGE (-) na POSITIVE CHARGE (+) zilizozalishwa hutenganishwa, ambapo positive charge hupelekwa na kujikusanya sehemu ya juu kabisa ya mawingu wakati Negative charge hujikusanya katika sehemu ya chini ya mawingu.
•Chaji hizi (Static charge - chaji zisizotembea) hua zina tabia ya kutafuta sehemu ya kutokea(escape or discharge) ili kukamilisha mzunguko wake na kuzalisha umeme - yaani hapa namaana kwamba sehemu yoyote yenye STATIC CHARGE, negative (-) huwa anatafuta mwenzake positive charge (+) sehemu yoyote alipo ili wakamilisha mzunguko - kitaalam tunasema ku-complete Circuit
•Hivyo basi NEGATIVE CHARGE zilizojikusanya sehemu ya chini ya mawingu angani huvutana na POSITIVE CHARGE zinazopatika katika uso wa dunia au ardhini. Ili postive charge zilizo ardhini kuweza kugusana na zile negative za angani hutafuta njia rahisi ya KIPITISHA UMEME (GOOD CONDUCTOR) ambayo mara nyingi ni kitu chochote kirefu kupita vingine kama vile MITI, MTU(akiwa sehemu tambarale isiyo na miti wala nyumba), NGUZO ZA SIMU au MINARA MIREFU na NYUMBA na MAGHOROFA MAREFU ambapo ndipo positive charge hizi hutumia kama njia ya kusafiria kwenda juu
•Negative charge kutoka katika mawingu zinazotafuta kuunganika na positive charge kutoka ardhini kitaalamu hufahamika kwa jina la STEPPED LEADER. Wakati positive charge zinazosafiri kutoka ardhini kwenda angani kuungana na Negative charge hufahamika kitaalamu kama STEAMER.
•Radi sasa ni umeme mkubwa unaoambatana na mwanga mkali na sauti kubwa sana za muungurumo ambazo hutokea baada ya Positive charge na Negative charge kuungana katika kukamilisha mzunguko. Kitaalamu mwanga huo huitwa LIGHTING BOLT au STRIKES.
•Radi hubeba umeme mkali sana unaokadiriwa kufika Voltage millioni moja (1000,000 volts)
2. KWA NINI RADI HUTOA SAUTI ZA MUUNGURUMO
•Radi inapopiga huzalisha joto linalofika 30000°c au 54000°F katika ile njia yake (hili ni joto kali mara tano zaidi ya joto linalozaloshwa katika uso wa jua).
•Wakati umeme huo wa radi unasafiri hutengeneza njia au shimo ambapo ndipo unapita, njia hii kitaalamu hufahamika kama LIGHTING CHANNEL.
•Hewa iliyopo kwenye njia hiyo huunguzwa na joto linalozalishwa na umeme huo wa radi na kusababisha hewa kutanuka na kusinyaa kwa haraka. Kitendo cha kutanuka na kusinyaa haraka kwa hewa baada ya kuunguzwa na joto kali huifanya hewa hiyo kulipuka ghafla na kuzalisha sauti kubwa
ambayo husikika pale hewa inapokua kwenye hali ya mtetemo( when the air vibrates).
•Sauti hii kitaalam hufahamika kama THUNDER. M
• Kimsingi Mwanga na Muungurumo wa radi ni vitu vinavyotokea kwa wakati mmoja ila kwa sababu mwanga husafiri haraka zaidi ya sauti, ndio maana huwa kwanza tunauona mwanga kabla ya kusikia muungurumo wa Radi.
•Sayansi inafafanua kwamba mwanga husafiri Maili 186,000 kwa sekunde (186,000 miles per second) wakati Sauti husafiri Maili 5 kwa sekunde (5 Miles per second).
• Unaweza kujua radi imetokea umbali gani kutoka uso wa dunia kupitia sauti inayozalishwa na radi hiyo. Mfano wataalamu wanasema itakuchukua sekunde tano ili kuweza kusikia sauti ya muungurumo wa radi iliyotokea katika umbali wa maili moja angani mara tu unapouona mwanga.
•Au kwa kurahisisha fanya hivi, hesabu sekunde mara tu unapouona mwanga wa radi mpaka pale unapousikia Muungurumo wa radi ili kuweza kujua umbali ambao radi imetokea. Hesabu ni kwamba kila sekunde moja inawakilisha Mita 343 kwenda juu. Hivyo sekunde 3 ni sawa na kilometers 1.
• Unapouona mwanga mkali na sauti kali sana yenye muungurumo mkubwa wa radi basi fahamu ya kuwa radi hiyo imetokea karibu sana na uso wa ardhi.
•Unapouona mwanga hafifu na sauti ya radi inayosikika kwa mbali au isiyosikika kabisa basi fahamu ya kuwa radi hiyo imetokea umbali wa kuanzia kilometa 20 na kuendelea.
3. KWA NINI RADI HUTOKEA KIPINDI CHA MVUA
•Radi hutokea kipindi cha mvua kwa sababu hewa yenye unyevu nyevu (Damp Air) au yenye maji maji hua njia rahisi ya kupitisha chaji za umeme.
4.AINA ZA RADI
•Kuna aina tatu za kutokea kwa radi.
•Aina ya kwanza
Ni ile radi inayotokea pale chaji hasi na chaji chanya za sehemu mbili ndani ya wingu moja zinapogusana. Kitaalamu hufahamika kama INTRA - CLOUD LIGHTING (IC).
•Aina ya pili
Ni ile radi inayotokea kati ya wingu moja na wingu jingine, pale chaji za wingu moja zinapo - discharge kuelekea wingu jingine. Kitaalamu radi hii hufahamika kama INTER CLOUD LIGHTING or CLOUD AND ANOTHER CLOUD (CC)
• Aina ya Tatu
Hii ndio hasa inayotuhusu na ambayo tumeizungumzia sana chanzo chake hapa, kwa sababu ndio inayoonekana na kuleta madhara katika maisha yetu. Hufahamika kama CLOUD TO GROUND LIGHTING (CG). Hutokea pale -(-ve) charge za mawingu zinapoungana na (+ve) charge kutoka ardhini kupitia njia rahisi ya kipitisha umeme kama vile miti, minara na majengo marefu.
5. MAMBO YASIYO YA UKWELI KUHUSU RADI
•RADI NI MNYAMA
Dhana hii ni uwongo ulioenezwa sana kipindi cha nyuma. Nakumbuka wakati nikiwa mtoto nilikua niliwahi sikia kwamba Radi ni mnyama mweusi mwenye miguu sita na ndiye huyo husababisha radi pale anapochukia. Dhana hii sio ya kweli Radi sio mnyama bali ni umeme unaozaloshwa angani katika mawingu ya CUMULONIMBUS.
•UKIVAA NGUO NYEKUNDU WAKATI WA MVUA UTAPIGWA NA RADI
Jambo hili pia si la kweli, nguo nyekundu haina uhusiano wowote na Radi na wala si Kipitisha umeme kiasi cha kua kivutio cha Radi. Hivyo huu ni uongo ambao unapaswa kupuudhwa.
•KONDOO HAPIGWI NA RADI
Jambo hili pia si la kweli, kuna uongo unaosambaa kwamba wakati wa radi kondoo huwa anapigana na radi. Kondoo kama yupo sehemu ambayo yeye ndiye njia rahisi ya radi kuingia ardhini pasi atapigwa na radi kama kawaida. Radi ina umeme mkubwa sana ambao hakuna kitu kinaweza kuuzuia zaidi ya kuwa na vifaa vya kuirahisishia kuingia ardhini.
• UKIWA UNAONGEA NA SIMU YA MKONONI WAKATI WA MVUA UTAPIGWA NA RADI
Jambo hili pia si kweli kisayansi na ni uzushi ambao umewahi kuenezwa katika mitandao ya internet. Simu ya mkononi haina sifa ambazo inaweza kua kivutio cha Radi, kwani ni kifaa kinachotumia umeme mdogo sana, na kina mabati kiasi kidogo sana ambayo hayawezi kuvutiwa na radi na haijaunganishwa na waya wowote.
Kuna uwezekano mkubwa wa kupigwa na radi ukiwa nje na uwe na simu ya mkononi au usiwe nayo.
• WATU WALIOPIGWA NA RADI WANABAKI NA UMEME WA RADI MWILINI HIVYO WASISAIDIWE
Dhana hii pia sio ya kweli, mtu akipigwa na radi hakuna umeme wowote unaobakia mwilini. Hivyo ni vema kumpatia huduma za haraka ikiwa ni pamoja na kimuwahisha hospitali.
6. JINSI YA KUWEZA KUJIKINGA NA RADI
• Jambo kubwa muhimu kulifahamu ni kwamba hakuna sehemu salama ukiwa nje itayokufanya uwe salama kujikinga na Radi pale mvua inaponyesha.
•Unashauriwa usitumie mwavuli wakujikinga na mvua katika mvua zinazoambatana na radi kwani mwavuli utakufanya kuwa kitu kirefu kupita vingine katika eneo ulipo na hivyo kufanya wewe pamoja na mwavuli wako kuwa njia rahisi ya radi kuingia ardhini.
• Endapo utakua nje wakati mvua za radi zikiendelea, epuka kusimama chini ya mti, kaa mbali na vitu virefu katika eneo ulilopo kama vile milingoti ya bendera au minara.
Maeneo mengi ya vijijini watu wanapokutwa na mvua na hakuna sehemu ya kujikinga na mvua, hukimbilia chini ya miti. Ni hatari sana kufanya hivyo kwa sababu ikiwa mti uliosimama chini yake utakuwa ndio mrefu kuliko kitu kingine chochote kinachopitisha umeme mahali hapo, basi radi itakamilisha muunganiko wake na ardhi kupitia mti huo na hapo ndipo utakapokutana na balaa kubwa la kifo ama majeraha makubwa.
•Epuka kukaa sehemu yenye uwazi isiyo na miti au kitu chochote kirefu mfano nyumba. Eneo lenye uwazi hapa tunalolizungumzia ni kama vile uwanja wa mpira, kwani ukiwa katika mazingira haya wewe ndiye utakua kitu kirefu kuzidi vingine. Kama radi ipo eneo hilo ni lazima tu itakupiga.
•Baada ya Radi kumalizika kaa ndani kwa muda wa dakika 30 zaidi kabla ya kutoka nje na kuendelea na kazi zako.
• Kama upo nje na umekosa sehemu salama ya kujificha basi chuchumaa chini huku ukiwa umebana miguu.
• Mara unapoona dalili za radi basi unashauriwa kukimbilia ndani ya nyumba zilizowekwa vifaa vya kuzuia Radi ( Lighting Rod or lightning arresters)
• Kukaa ndani ya gari kunaweza kukuzuia kupigwa na radi, lakini unashauriwa kufunga vioo na kutokushika kitu chochote chenye asili ya chuma ukiwa ndani ya gari, hapo utakua salama.
• Endapo eneo ulilopo kuna radi au dalili za kutokea kwa radi basi unashauriwa KUTOKUFANYA mambo haya, Usinawe mikono kwa maji, usifue nguo, wala usiogelee au kuoga muda huo.
• Zima vifaa vyako vyote vya umeme kama vile TV, Radio, computer n.k, na uchomoe nyaya zilizounganishwa kwenye chanzo cha umeme, na fanya haya kabla radi hazijaanza kupiga, usichomoe waya wakati radi inapiga.
• Usitumie Simu za mezani , (kama vile zile zitolewazo na TTCL zilizounganishwa na waya kutoka kwenye nguzo) wakati wa mvua za radi kwani kuna uwezekano mkubwa ukapigwa na radi.
• Ukiwa ndani ya nyumba wakati wa mvua za Radi, epuka kukaa karibu na dirisha, bafuni, kwenye masinki ya maji, Television, Radio, simu za mezani na Computer, kwani ukiwa karibu na vitu hivi una uwezekano mkubwa wa kupigwa na Radi.
•Epuka kukaa sehemu zenye miinuko kama vile vichuguu au milima kwani uwezekano wa kupigwa na Radi ukiwa eneo hilo ni mkubwa sana.
• Epuka kuvaa vitu vyenye asili ya chuma kama vile cheni, mikifu na hereni wakati radi.
TOA MAONI YAKO KISHA
Tags