Ndoa Nyingi za Kizazi Hiki Zinavunjika Kwa Sababu za Kijinga, Nguvu ya Mwanamke Katika Ndoa

POWER OF A WOMAN IN MAKING THE MARRIAGE WORK!

1st Lesson SOMETIMES A WOMAN WINS BY LOOSING! Unaweza mwanamke ukajiona umepoteza kitu ila in reality umeshinda! Na unaweza kuona umeshinda ila in reality umepoteza. Usiendekeze hisia za moyo zinavokuongoza na wapambe! Tumia akili na busara zaidi! Mfano unapewa data mumeo yuko guest kafumanie, kuliko kwenda na kumuita shigongo kuvunja utu wako na wa mumeo na kutia doa maisha yenu shukuru tu taarifaa, mpe mumeo benefit of the doubt sali kwa Mungu wako. Kuchapiwa ni siri ya ndani indeed! Usimchunguze mumeo kama CIA au KGB sababu ukitafuta sanaa kitu utakipataaa! Manake wanawake kuna tabia unamfatilia una withold eveidence hiku unaikusanya hadi uhakikishe siku ukimsomea mashtaka hana pakutokea ushahidi unatosha kuconvict. Hahahaaaaaa!

2nd Lesson! BY NATURE MARRIAGE IS SELF DESTRUCTORY, LOOK FOR SOLN TO MAKE IT WORK! Yaani nature yenyewe mambo ya kumkinai mwenzio, kutamani vipya, ni natural tu, hayahitaki hata sababu, sasa baada ya kuwa mtu wa lawama, kulaani kwanini mambo kama hayo yawatokee, kumuona mwenzio hana shukrani, spend more time kudeal na situation kuliko mwenzio. Kama uzazi umekubongesha work out, acha kula hivo. Kuliko kudemand the impossible kuwa sababu umemzalia akupende hivo hivo kwenye jimwili jipya sio rahisi. Shirikiana kutafuta soln.

3rd Lesson USISAHAU HATA SIKU MOJA AT A POINT LIFE YOU WERE HIS NUMBER ONE NDO MAANA AKAKUOA! Hata kama anakunyanyasa saivi, heshima haipo, anachepuka, labda wewe upo number 100 saivi not even once dont let you forget once upon a time you were his number 1, he married you, yes you na mapungufu yote yako, not Lily the cutest, mima the big as.s, Rose the beauty queen etc, wote aliwaona yet still akakuona wewe ugly betty or whatever! Tatizo ni kujisahau, wakati anakuoa you might have been ugly still lakini una heshima, upo humble, etc sasa umo ndani ndo unajifanya king kong atakwambia nini si ushindani hamna! Ukiona mambo magumu rudi back in the days ujiulize ulimloga vipi wakati ule umloge tena!

4th Lesson UTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILE ILE! Unakuta mtu unamuacha mumeo kisa muhuni ana michepuko? Mwanaume gani asie na michepuko? Hahahaaa! Utamuacha wa kwanza utatafuta 2, wembe ule ule, utahangaika mpaka basi! Kabla hujamuacha mumeo kisa michepuko jiulize nani hachepuki utaempata? Au mimeo hela hana! Hata unaemkuta nazo zaweza kusiha vile vile. Tulia vumilia unyolewe. Wenzio wote wametulia wewe unajilegeza! Ifike mahala fumba macho uombe Mungu siku ziende maana hata ukisema uende kwingine mwendo ule ule! Unamuacha mumeo unaanza kuiba wa wenzio! Akili matope hayo?

5th Lesson KABLA HUJAPANIC KWA JAMBO MOJA KUMBUKA MEMA YAKE ELFU MOJA NDO UAMUE KUHUSU HIKO KIMOJA! Mtu kakuoa miaka 5, anakupa yote utakayo, anakiabudu malkia wake, hakuna unachokosa, shabash kateleza kidogo shetani kampitia sisi wote binadamu kakusoea kachepuka one time! Basi wewe. Unasahau mema yoooooote ya 5 years huko kumshika ndo unafunga mabegi na kutokomea! Khaaaaa! Au mmeishi vizuri miak 7, mwaka huu ndo kabadilika, japo uvumilie na kuomba atambue makosa na kujirudi miaka yote 7 watia kwenye dustbin, unashupalia matendo yake mwaka huu na kudai talaka! Sasa na mwanaume mda mwengine nae anakereka anaona kama wema wake wa miaka 7 sio issue basi nendaa tu! Power of love sio kufaidi goodtimes ni kuhimili mikimikiki! Wapambe nuksi kina lara 1 tunakutia ndimu ondoka bwanaa, kwanini afanye hivo, ndo unakole kweli kweli. Usiruhusu tendo moja la kijinga likupotezee 7 yrs of your life n hard work! Kwani ukisamehe hilo fumanizi utababuka? Vitakuuma vitapoa mnaanza upya! Hatoki mtu inaitwa! Atafanya visa wee akikuona mkomavu atachoka mwenyewe!

6th lesson! JIFUNZE KULET THINGS GO! Sio basi ukimfumania mara moja kila akikosea kidogo unamshikia kooni ile ugoni wa mwaka juzi. Kitu kidogo unaretrieve file! Au ulimsaidia mwaka juzi alipokwama, akikunyima hela kidogo unakumbushia, mwaka juzi fyoko fyoko! Daaah! Sio issue. Inatakiwa uwe mkomavu ukisema umesamehe kitu basi ndo unakizika kooni forever! Haukitaji tena! Unamuepusha shaitwani kukaa kati kati yenu kila wakati! Unavomsamehe mara nyingi inaondoa hata ile ladha ya kukusoea tena! Sababu anajua utamsamehe na wala hutomuuliza tenaaa! Mwenyewe anajistukia. Ananza kuona kweli huyu si binadamu wa kawaida, labda namtendea ndivo sivo.

7th lesson! MUME NAE BINADAMU LOLOTE LINAWEZEKANA! Usiwe na expectations kubwa sanaaaaaa! Ukamuona yule malaika labda hawezi kukosa. Aaaaah! Wapi! Jua tu yule binadamu kupitiwa inawezekana pia, na hata akipitiwa unajua umejipanga kusort hizo issue out kuendeleza libeneke! Ila kama ndo ulikuwa unamuona mungu mtu, siku akiteleza waweza kuga kwa pressure! Wakati cha ajabu hamnaa mbona! Kwani ye wa kwanza kufanya hivo? Au wa mwisho? Hamnaaaaa!

By Lara 1
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu upuuuzi manake hata Lara 1 katumwa kuuandika!
    Upuuzi mkubwa tena usenge wa hali ya juu! Hivi wanawake wa Afrika tumelogwa na nani?
    Ndoa haikua na maana ya kuishi kwa mateso! Uvumilivu wa kutendewa mabaya ni Yesu tu aliweza kuvumilia! Mohammed mwenyewe alishindwa akaanzisha jino kwa jino!
    Ndoa ni UPENDO si kuvumilia mateso! tena yanayofanywa kwa makusudi na jinsia moja WANAUME!
    Kama uvumilivu ni rahisi na wanaume wavumilie wake wavivu, wachafu, wasioweza kupika vizuri, wenye gubu na Malaya!
    Unachotaka kutendewa basi na wewe tendea mwenzako!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nooooooo nadhani hukuielewa ile dhana nzima ya mwandishi. Basically kitu anachojaribu kukuambia ni kuwa if things goes wrong in a relationship still you have that chance of settling things down rather than running into conclusions or give up. Sasa wewe unafikiria mwandishi yuko biased. No haiko hivyo. Jaribu kusoma na kumwelewa vizuri. Jamani tuwe na utaratibu wa kuwa patient na tabia za watu na pia tujenge utamaduni wa kupeana second chances dah

      Delete
    2. mmh, kwa sisi wagongo labda useme kupeana 50th chance! maana mwanaume anacheat weeeee, leo na mke wa jirani, kesho na dada wa kazi mwezi ujao na mfanyakazi mwenzie huko ofisini kwake etc, na bado yoote hayo ni irresponsible kwa nyumba, mwanamke ufanye kazi ulipe kodi ya nyumba, ada za watoto, chakula, bills zote. Na bado Mnaambiana mvumile tu! du wanawake wa kiafrica kweli aliyeturoga kafa

      Delete
  2. Hii ni namna ya kumpumbaza mwanamke na kumnyanyasa kiakili na kihisia!
    Hizo points zitumike kwa wanaume! Ni rahisi kunyooshea kidole mwingine afanye ila wewe binafsi huwezi hata moja! Kama ndoa ni institution ya kinafiki wacha zivunjike, hata Biblia imesema ndoa isivunjwe ila kwa UZINZI!
    Ninyi marriage concillors uchwara mnajitia eti akicheat, msamehe mvumilie! Tena bila haya shenzy zenu mnawaambia wanawake ndiyo wavumilie! Wanaume je?
    Mwanamke avumilie UFUKARA wa mwanaume halafu mnaongeza na moto mwingine wa uzinifu?
    Thubutuuuuuu labda muoe vibibi vya 47!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana dah. Mdau inavyoelekea una hasira sana. Sidhani kama huyo mwandishi anajaribu ku suppress akili za wanawake. Kwani kosa la ku cheat among spouses lina uzito wake tena pengine usiovumilika lakini linapotokea jambo kama hilo basi ni lazima zitumike busara kubwa katika kulitatua tatizo hilo.

      Delete
  3. Lara 1 nimekushusha sana! Jamii forum huwa una rock na mada hot zinazowapa adabu wanaume vilaza! Zinawaweka kwenye mstari na kuwa discipline na ndiyo sababu wanatoka mapovu vibaya sana.
    Unajua kiafrika mwanaume haonywi wala kuulizwa wala kuekekezwa so wanapokutana na threads zako pumbu zinawabana wanabaki kupovuka!
    Ila hii mwambie aliyekutuma ailete mwenyewe aone tutakavyomtoa kamasi! next time usiwe masogange kufanyika punda wa kubebea wengine mizigo hatarishi!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau huna sababu ya kumshusha mtu based on her/his personal opinion. Na wala hatuko hapa kukomoana au kukomeshana. Ni jukumu letu sote kama wadau kuelemishana katika mada mbali mbali bila ya kuwa biased ili kuufurahisha upande mwingine au kuifurahisha gender nyingine.

      Delete
  4. Lara 1 nimekushusha sana! Jamii forum huwa una rock na mada hot zinazowapa adabu wanaume vilaza! Zinawaweka kwenye mstari na kuwa discipline na ndiyo sababu wanatoka mapovu vibaya sana.
    Unajua kiafrika mwanaume haonywi wala kuulizwa wala kuekekezwa so wanapokutana na threads zako pumbu zinawabana wanabaki kupovuka!
    Ila hii mwambie aliyekutuma ailete mwenyewe aone tutakavyomtoa kamasi! next time usiwe masogange kufanyika punda wa kubebea wengine mizigo hatarishi!

    ReplyDelete
  5. Ovyo badala ya kuandika madhara ya michepuko unaelezea ionekane ya kawaida na ni jambo likubaliwe huna tofauti na wahamasisha ushoga wewe. Eti he loved u once upon a time sawa he loved me but no longer inlove with me nivumilie aniue then mseme y sikutoka khaa au utakuja kunipa taji ya uvumilivu na hiv yangu kitandani. Eti oh ana mapungufu kwani pungufu ni uzinzi pekee? B inasrma dhambi zote ni juu ya mwili ila uzinzi ni mdani ya mwili. Ndoa ni starehe msitake ionekane ni sehemu ya mateso na wapo wasiocheat wapo na wakicheat watapewa adhabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah kwa kweli mdau gadhabu zako sio mchezo. Nadhani siku ikitokea ukamfumania mmeo siku hiyo utaua kabisa dah hahaha

      Delete
  6. hivi huyu lara 1 ni mwanamke kweli,ameyawza hayo au kahongwa awasafishewanaume.hivi unaujua uchungu wakusalitiwa au unauskia,usiwatetee hawa wapuuzi wanatake advantage kwenye ishu kama hizo,wanazisoma wanajiona wako sawa ila sisi tukikosea kidogo wanatusumbua pumbavu zao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimejaribu kumsoma mwandishi na sioni wala kuamini kama ni kweli ana support michepuko bali nadhani anachojaribu kutuambia ni kuwa in case of such a scenario try to work things out kwani binadamu ni wale wale. Lakini bado nashindwa kukuelewa wewe mdau ni wapi unapopasimamia kwa sababu hoja zako nyingi zimeelekea ku criticise hoja za mwandishi na ku blame yeye kuwa pengine ametumwa lakini unashindwa kutueleza ni kitu gani kifanyike ili kupunguza au pengine kulimaliza kabisa tatizo la aina hiyo. Ndugu mdau tungependa kujua ni nini mtizamo wako juu ya hilo tatizo.

      Delete
  7. Nikuulize wewe unaye reply hapo juu nini kifanyike ili kupunguza tatizo la mkeo kutiwa nje ya ndoa? Tutumie busara ili kudumisha ndoa! Wafundishe na wanaume wenzio namna ya kuhandle mke mchepukaji bila kuathiri ndoa!

    ReplyDelete
  8. Mke wako akicheat ukimfumania mnunulie vitz na mjazie mafuta full tank, ukimfumania mara ya pili mpe Kluger! Atajirekebisha tu jinsi unavombembeleza kwa zawadi mdau uliyeuliza hapo juu!

    ReplyDelete
  9. wala mwandishi hajakosea kitu hapo, Mimi Ni mwanamke lkn nimemwelewa fresh kabisa, sisi wanawake tunachuja sana (ukubali/ukatae) ukweli haupingiki, wanaume hawachoki hata kibomba kitoe maji ya Tz mzima bado anakua poa tu, wanawake tutulie chini kwani tangu tumeanza kuwafumania na kuwadhalilisha ma BF wetu na waume zetu ndio wameacha? ndio kwanza halo inazidi kuwa mbaya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad