Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa hana mashaka na kuwa Rais Magufuli ataendelea kushikilia nafasi hiyo, kwani hana mpinzani kutokana na utendaji wake wa kazi.
Makonda ametoa kauli hiyo leo Februari 25, 2020, wakati akifungua mkutano wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC), uliowakutanisha Wabunge, Madiwani, Mameya pamoja na Wakuu wa Wilaya kwa lengo la kujadili na kutokomeza kero mbalimbali ndani ya Mkoa huo.
"Rais atakayeendelea kuongoza Taifa hili anajulikana, kuna siku nikamsikia mtu anajitangaza kule atachukua fomu ya kugombea Urais, nikasema wakimpitisha huyu kwenye chama chao mimi nitamuomba Dkt Magufuli nihangaike naye, huwezi ukamchukua Dkt Magufuli ukamshindanisha na kibaraka anayesimama kwenye jukwaa eti naye anagombea Urais wa nchi" amesema Makonda.
Hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema kuwa anayo nia ya dhati ya kugombea Urais na kuiongoza nchi, endapo wenzake wataridhia yeye kupeperusha bendera hiyo.
Hivyo wazamiaji pia wanaweza kuchukua fomu za Uvira au Nyakabiga. Hee hicho chama cha Twita atagombea Fezibuku
ReplyDeleteau nniyo kujishaua ili apate teke kwamba Tanzania Hawakumpekenyua..?Makonda nakuamini. Shughuli na waiotoroka
Makambini na Kublend inn. Hawa hwana Dhamira nzuri nna Hawaitakii mema Nchi yetu. Mifano iko wazi na bayana.
Ni Lazima waelewe Tanzainia ni ya Watanzani Ukarimu wetu isiwe Sababu.
Huyu alikwwenda Kwa Mbuta Nanga kutafuta Mgao.
ReplyDeleteBaada yakujulikana MAMLUKI. Ikabidi abadilishe gea angani mpaka kwa Baliki akaambulia Lawyer wa UHAMIAJI.