Pele afunguka kuhusu hali yake ya kiafya



Aliyekuwa mchezaji soka maarufu Brazil amezungumza kwa mara ya kwanza tangu mwanawe wa kiume alipodai kwamba kwasasa huwa hayuko radhi sana kuondoka nyumbani na kuongeza kuwa hali yake ya afya ni jambo la kawaida kwa mtu mwenye umri kama wake.

Mtoto wa Pele Edinho alisema bingwa huyo mara tatu wa kombe la dunia, 79, anaona aibu kutoka nje ya nyumba yake na pia anahitaji usaidizi wa magongo kutembea kwasababu ya matatizo yake ya kiafya.

Hatahivyo, Pele anayetambulika kuwa mchezaji bora amesema: Niko sawa. Ninaendelea kukubali hali yangu kiafya kwa namna nzuri zaidi na nia yangu ni kuendelea na maisha yangu kama kawaida."

Pele alivunja rekodi ya dunia kwa kufunga magoli 1,281 ikiwa ni rekodi ya duniani katika mechi 1,363 wakati wa kipindi chake cha miaka 21 katika kandanda, ikiwemo magoli 77 katika mechi 91 akiichezea Brazil.

Mwaka 2015, alifanyiwa upasuaji wa tezi ya kibofu na pia mwaka jana alipelekwa hospitalini akiwa anaugua maambukizi ya njia ya mkojo.

Marafiki wa dhati wa Pele aliyekuwa mchezaji wa Santos na New York Cosmos walisema kwamba Januari mwaka huu ni miongoni mwa miezi ambayo alikuwa na shughuli nyingi za kufanya.

Upigaji picha na kazi ya ufadhili anayofanya, Pele anashirikiana na mwelekezi mmoja wa Uingereza kutengeneza makala kuhusu maisha yake wakati anacheza soka.

"Hata katika ratiba yenye shughuli nyingi bado ninatekeleza majukumu yangu ," amesema hivyo katika taarifa aliyotoa.

"Kuna siku zinakuwa nzuri na nyingine mbaya. Hiyo ni kawaida kwa watu wenye umri kama wangu. siogopi lolote, nimeazimia na ni mwenye matumaini na kile ninachofanya."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad