Huko nchini Ukraine, yamefanyika maandamano kupinga raia wa nchi hiyo waliokuwa nchini China kurejeshwa nchini Ukraine kufautia kuzuka kwa kirusi kipya cha Corona (Kovid-19).
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na vyombo vya Ukraine, raia 45 wa Ukraine na wengine 27 wa kigeni, jumla ikifanya watu 72 waliwasili mjini Harkov nchini humo wakitokea Wuhan kwa usafiri wa ndege .
Watu hao 72 baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege walichukuliwa na mabasi 7 ili kupelekwa katika kituo kimoja cha afya katika mji a Novie Sanjari, wakiwa njiani kuelekea katika kituo cha afya walizuiwa na baadhi ya raia wa Ukraine kuingia mjini humo.
Watu hao waliokuwa na hofu kwamba wataletewa virusi vya Corona walianza kuyarushia mawe mabasi hayo.
Polisi ikabidi waingilie kati kujaribu kuwatuliza waandamanaji hao.
Waziri wa afya Zoriana Skaletska kupitia mtandao wa Facebook amesema kwamba wamechukua tahadhari za kutosha, na hivyo watu hao watatengwa kwa muda wa wiki 2 kwa ajili ya uchunguzi.
Skaletska alisema kwamba mchakato huo wa kuwahamisha watu hao umekidhi vigezo vya Umoja wa Mataifa.