"Rais Magufuli Ameniliza Mara Mbili"-Dully Sykes


Mkongwe wa BongoFleva Dully Sykes, amesema Rais Dkt John Pombe Magufuli, amewahi kumliza mara mbili kutokana na uongozi wake na utendaji wake wa kazi.


Upande wa kulia pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kushoto ni msanii Dully Sykes

Dully Sykes ameleza hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kila siku ya Jumatatu-Ijumaa kuanzia 7:00 mchana hadi 10:00 jioni, ambapo amesema Serikali ya awamu ya Tano ni kali na Rais Magufuli ana huruma sana kwa wananchi wake.

"Serikali ya awamu ya Tano ni kali sana kwa sababu ya matukio yaliyotokea huko nyuma na ina mtazamo tofauti na sisi tunavyodhania, pia kwa upande wangu mimi Rais Magufuli ana huruma sana natamani hata aongezewe miongo mingine mitano ili aweze kuongoza nchi yetu" ameeleza Dully Sykes.

SOMA HABARI HIZI KUPITIA APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD > HAPA



Aidha mkongwe huyo wa muziki ameendelea kusema "Mimi naogopa siasa, Magufuli ameniliza mara mbili kwa sababu ya utendaji na uongozi wake wa kazi, mara ya kwanza alivyoniliza kuna mwanamke alikuwa anadai haki zake akatoa ruhusa asikilizwe, mara ya pili aliniliza alipotoa Milioni tano kwa yule mama wa hospitali ya Muhimbili ili alipie kutoa mwili wa mama yake".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad