Rais Magufuli Kuzindua Rasmi Wilaya Ya Kigamboni Leo


Rais Magufuli leo February 11 kuanzia Saa Mbili Asubuhi anatarajiwa Kuzindua Rasmi Wilaya Mpya ya Kigamboni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika Uzinduzi huo wa Kihistoria.

RC Makonda amesema hafla ya Uzinduzi huo inatarajiwa kuanza Saa Moja Asubuhi kwenye Viwanja vya Mkuu wa Wilaya ambapo Rais Magufuli atazindua Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya, Jengo la Halmashauri na Majengo ya Hospital ya Wilaya ya Kigamboni.

Uzinduzi huo unakuja wakati muafaka ambao Tayari Serikali imefanya juhudi kubwa za Maendeleo katika Wilaya hiyo kupitia Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Barabara za Lami, Ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati, Huduma za maji, Elimu pamoja na huduma zote muhimu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad