Rais Trump Ajitapa "Tumemuua Kiongozi wa Al-Qaeda"


Rais Donald Trump amesema Marekani imemuua Kiongozi wa Al-Qaeda katika eneo la Rasi ya Urabuni (AQAP), Qassim Al- Raymi, kwenye oparesheni maalum iliyofanyika Yemen, Trump hajasema ni lini wamemuua.

" Qasim al-Raymi (aliyeongoza kikundi cha Jihad tangu mwaka 2015) na timu yake walipanga mashambulizi kadhaa kwa Marekani na Majeshi yake, na kufanya uhalifu mwingi wa kibinadamu Yemen"- Trump

“Kifo chake kinaendelea kudhoofisha AQAP na Kundi la al-Qaeda kwa ujumla na kufanya tuendelee kukaribia kuondosha vitisho vya makundi haya yanayohatarisha usalama wa Marekani" - Trump

Marekani imesema inalichukulia kundi hilo la AQAP kama tawi hatari la mtandao wa Al Qaeda ulioanzishwa na Osama Bin Laden.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad