RPC afunguka sakata la polisi kuwapiga risasi wafugaji Misungwi, mmoja auawa



Mfugaji John Lugata (30) Mkazi wa Kijiji cha Misasi ameuwawa na wengine wawili kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari Polisi wilayani Misungwi mkoani Mwanza kufatia vurugu iliyojitokeza baada ya yeye na wenzake (wachungaji) kuvamia na kuwashamburia wafanyakazi wa shamba la Uzalishaji Mifugo la Taifa lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi.

Tukio hilo limetokea Feburuari 16 mwaka huu Majira ya saa 10:00 jioni katika eneo la Kijiji Mabuki na Kata ya Mabuki ambapo lilidaiwa kuwa kundi la wafugaji limekuwa na mazoea ya kuingiza mifugo (mbuzi, ng’ombe na kondoo) kwa ajili ya malisho huku wakifanya vitendo vya uhalifu kwa kuwapiga wafanyakazi wa shamba hilo kwa mawe na siraha za jadi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Muliro Muliro amesema kuwa katika tukio hilo mfugaji Lugata akiwa na kundi la wenzake walivamia eneo la shamba hilo kuingiza mifugo yao kwa malisho huku wakiwashambilia kwa mawe na siraha za jadi baadhi ya wafanyakazi waliojaribu kuwazuia.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa wafanyakazi wa shamba la Mabuki za kuwepo uhalifu huo, askali Polisi kutoka Misungwi walikwenda eneo la tukio na kukuta hali mbaya ya vurugu na walipojaribu kuwatuliza kwa kupiga mabomu ya machozi ya kutawanya kundi la wafugaji hao, lakini waliwashambulia askali Polisi kwa kuwarushia mawe kwa kutumia makombeo,”alisema.

Kamanda Muliro amesema kwamba katika majibishano hayo kati ya Polisi na wafugaji askali Polisi wawili wenye namba J 2395 PC Majani ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia kwa kupondwa jiwe na H 6418 PC Mzee ambaye alijeruhiwa sehemu ya mkono wa kulia kwa kupigwa jiwe huku wafugaji Hangwa Masanja (28) na Benjamin Musa (32) nao walijeruhiwa kwa mawe.

“Wakati wa vurugu hizo ambapo tayari wafanyakazi wa Mabuki walikuwa wamefanikiwa kukamata mifugo 300 lakini wafugaji walikuwa wamefanikiwa kutorosha ng’ombe 124 huku ng’ombe 176 wakilipiwa faini ya Sh 100,000/ kwa kila ng’ombe mmoja ambazo tayari walikuwa wamelipa baada ya vurugu kutulizwa na Polisi,” alisema.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL


“Vijana wasitumike kwa kukodishwa ili kuvunja sheria kwa ahadi za kulipwa ujira wa fedha na wanaowakodi kwa kusaidia kutorosha mifugo iliyokamatwa ikiingia hifadhi ya Shama la Mabuki kinyume cha taratibu na sheria hivyo watakamatwa na kushitakiwa kwa kuvunja sheria kutokana na kufanya vitendo vya uhalifu,”alisisitiza.

Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ikiwemo kuwasaka na kuwakamata watu waliovamia, kujeruhi askali Polisi na kuvunja sheria na badae kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad