RPS Singida: Nilinukuliwa Vibaya Kuhusu Kifo cha Kiongozi wa CHADEMA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Sweetbert Njewika, amekanusha kauli yake iliyodai kuwa dereva bodaboda aliyeuwawa mkoani humo, hakuwa kiongozi wa CHADEMA na kusema kuwa alinukuliwa vibaya.

Akizungumza leo Februari 28, 2020 kamanda Njewike amesema kuwa walioitoa taarifa hiyo hawakumnukuu vizuri kwani yeye hakutoa taarifa ya moja kwa moja kuwa Jonas hakuwa kiongozi wa CHADEMA.

"Nilichosema kwamba yule ni bodaboda inawezekana anafanya kazi nyingine, sikukanusha kwamba yule siyo kiongozi wa CHADEMA, naomba mninukuu vizuri na ndicho nilichokisema" amesema Kamanda Njewike.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa Alex Joas alikuwa  ni Katibu wa CHADEMA Manyoni Mashariki.

Alex Joas inadaiwa kuwa mwili wake uliokotwa mbugani mbali na barabarani, ukiwa na majeraha ya kuchomwachomwa na kitu chenye ncha kali na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad