Saudi Arabia waweka mzigo Dola 517 milioni pambano la Fury, Joshua



Umesikia mzigo ambao Saudi Arabia wameweka mezani kwa ajili ya pambano la Tyson Fury dhidi ya Anthony Joshua au Deontay Wilder? Ni kufuru.

Ishu kamili iko hivi, familia ya kifalme ya Saudi Arabia inataka kuona pambano lijalo la Fury linafanyika nchini mwao iwe dhidi ya Joshua au Wilder na kama uwajuavyo Waarabu wanapotaka jambo lao pesa hutumika kufanikisha.

Si unakumbuka kilichotokea kwa Joshua na Andy Ruiz Jr? Dola 70 milioni tu zilitosha kupeleka pambano lao la marudiano Saudi Arabia na kuzipotezea kelele zote za walioponda kitendo hicho. Pesa iliongea. Katika pambano hilo Joshua aliingiza Dola 60 milioni milioni wakati mpinzani wake, Ruiz Jr alipiga Dola 10 milioni - pesa ambazo zilikuwa ndefu zaidi kwa kila mmoja katika historia yake ya ngumi. Si mchezo.

Inaonekana shoo ya Joshua na Ruiz Jr iliwakuna sana na sasa Saudi Arabia wanataka burudani nyingine ya ngumi, lakini safari hii akili yao yote ipo kwa Tyson Fury au The Gypsy King kama anavyojulikana na wengi.

Kichapo alichokitoa kwa Wilder kimewakuna na wanataka kuona pambano lake lijalo linachezwa Saudi Arabia hasa lile la kuunganisha mikanda dhidi ya Joshua, na ndiyo maana mezani wameweka Dola 517 milioni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad