Serikali ya Kenya Yamsaka Harmonize Kufuatia Deni ya KSh 200k



Msanii Harmonize aliliharibu gari aina ya Range Rover Sport na kukataa kufidia licha kuahidi kufanya hivyo awali

Wasimamizi wa shoo wamemfumgulia kesi ambako wanadai fidia hiyo

Meneja wa Harmonize Mjerumani alithibitisha kisa hicho  na kuwaahidi mashabiki wake kuwa walikwisha malizana na kisa hicho

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemfungulia kesi msanii Harmonize wakitaka kumkamata kuhusiana na deni ya Ksh 200k.

Leo limethibitisha kuwa msanii huyo aliliharibu Range Rover la promota wa Kenya na kukataa kumfidia licha ya mkataba wa awali wa kufidia.

Kwa mujibu wa jarida la Global Publishers, Harmonize alikuwa amealikwa kupiga shoo mjini Mombasa Kenya na alipaswa kulipwa KSh 1 milioni.

Kando na hivyo, msanii huyo aliomba kupewa gari aina ya Range Rover ili kutumia mjini humo kuitangaza shoo hiyo.

Wasimamizi wa shoo walikaidi ombi hilo wakidai kuwa huenda gari hilo lingeharibika.

Harmonize alisisitiza na hata kuahidi kulipia na hatimaye akapewa gari hilo.


Harmonize alianza mzunguko wake mjini Mombasa katika kuitangaza shoo aliyopangiwa kupiga, kutoka na umaarufu wake, mashabiki walijaa katika eneo la Mama Ngina Drive na hapo wakaiharibu Side Mirror ya gari hilo.

Uharibifu huo ulimkasirisha wasimamizi wa hafla hiyo na kuamuamuru afidie suala ambalo alikubali bila pingamizi.

Wasimamizi hao waliamua kuwa watamlipa KSh 800k badala ya KSh 1 milioni suala ambalo Harmonize alilikataa na hivyo akaamua kutoroka nchini bila kupiga hiyo shoo.


Waandalizi wa shoo hiyo sasa wanamtaka Harmonize kulipia fidia ya gari hilo pamoja na hasara iliyotokana na kuavya kwa shoo hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad