Shetta Afunguka Mondi Kumpora Mama Qayllah
0
February 25, 2020
SHETTA ndilo jina linalompa ugali wa kila siku. Lakini Nurdin Bilal ndilo analotumia kwenye kitambulisho cha Nida, hati ya kusafiria, vyeti vya shule, cheti cha kuzaliwa, leseni za magari na biashara zake na utambulisho mwingine wa kiserikali.
Shetta ni kichwa kingine kikali cha Bongo Fleva. Jamaa alitisha mno baada ya kuachia ngoma yake ya Nidanganye iliyokuwa na mashairi tata, akishirikiana na kiranja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Baadaye aliachia ngoma kama Mama Qayllah, Kerewa, Namjua, Shikorobo aliyomshirikisha KCee wa Nigeria na nyingine nyingi.
OVER ZE WEEKEND inamsogeza kwako Shetta katika spesho intavyu kuhusu maisha yake halisi na mkewe, Leyla ambaye wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miaka 10 na kubahatika kupata watoto wawili; Qayllah na Qamrah. Shetta anafunguka vitu vingi likiwemo suala la Diamond au Mondi kumpora Mama Qayllah;
OVER ZE WEEKEND: Shetta hatujafanya intavyu siku nyingi, lakini moja ya vitu unavyozungumziwa ni video zako mbalimbali. Je, unatumia gharama kiasi gani kutengeneza video zako?
SHETTA: Mara nyingi huwa sipendi kutaja gharama za video au audio ninazozitumia. Niliwahi kutaja, halafu ikasababisha mambo mengi ya kuonekana tunaongeza sifuri mbele. Mtu unaweza kutaja kwa nia nzuri tu, lakini ikawa vinginevyo.
OVER ZE WEEKEND: Kuna maneno mengi kuwa video yako ya Ngoma ya Namjua, ulikopi My Number One ya Diamond au Mondi na Bado ya Harmonize, ni kweli?
SHETTA: Hazifanani. Nafikiri labda ni kwa sababu ya kutumia boti na ndege ambazo zimetumika kwenye My Number One na Bado. Lakini inategemea vitu hivyo vimetumikaje. Mimi sioni ufanano wowote.
OVER ZE WEEKEND: Hadi sasa una hazina ya ngoma ngapi zilizorekodiwa na kutoka na ambazo hazijatoka?
SHETTA: Ni nyingi sana. Kwa mfano mpaka sasa nimeachia jumla ya ngoma 17 na nyingine tatu zilizovuja. Mimi huwa sipendi kuachia ngoma kila wakati, zipo nyingi bado, nasikilizia kuziachia.
OVER ZE WEEKEND: Kuna tetesi kuwa huwa unakataa kolabo, je, ni kweli?
SHETTA: Si kweli, huwa sikatai kolabo kwa sababu hata mimi nimetoka huko. Hasa kwa wasanii wachanga, lazima niwasikilize na kufanya nao kazi. Ila kinachoniboa ni kwamba sipendi kukutana na mtu ambaye ninampa nafasi, halafu ninagundua hana kipaji. Huwa ninainjoi sana ninapokutana na mtu ambaye ninampa nafasi na yeye ananipa nafasi.
OVER ZE WEEKEND: Katika kipindi chote cha muziki wako, umepata mafanikio gani?
SHETTA: Ninamshukuru Mungu nimepata vitu vingi sana. Unajua ukishakuwa maarufu unapata utajiri mwingi tu, ukiachilia mbali fedha.
Ukirudi nyuma ya mwaka 2009, Shetta alikuwa siyo huyu wa sasa. Mafanikio yapo na sitaki kusema uongo mbele ya Mungu kuhusu hilo.
OVER ZE WEEKEND: Mbona hatukuoni kwenye shoo?
SHETTA: Shoo zipo nyingi tu na za kutosha. Kila ninapoachia ngoma huwa ninapata shoo za ndani na nje ya Bongo. Ila kuna wakati unaamua tu kupumzika.
OVER ZE WEEKEND: Nje ya muziki tunajua Shetta unafanya vitu vingi hasa biashara. Je, unawezaje kubalansi muda kufanya mambo yote hayo kisha unaongezea na familia?
SHETTA: Ni kweli mbali na muziki ninafanya biashara ndogondogo. Kufanya vitu vingi inasaidia wanangu waende shule na kama mtu una shauku ya kufanya mambo, basi huwezi kukosa muda.
OVER ZE WEEKEND: Wasanii wengi sasa hivi wanatembea na mabaunsa na wewe ni mmoja wao, inasaidia nini?
SHETTA: Ulinzi ni muhimu sana. Sehemu yoyote kwenye mazingira ya watu wengi, mara nyingi huwezi kujua nani anakuja, nani mzuri au mbaya. Hivyo kwangu mimi, sehemu yoyote ambayo ninahisi kwamba usalama wangu utakuwa mdogo, ninahitaji kujilinda.
OVER ZE WEEKEND: Pamoja na changamoto nyingi, lakini umedumu kwa zaidi ya miaka kumi na Mama Qayllah. Je, unaweza kuoa mwanamke mwingine?
SHETTA: Siwezi wala sifikirii kabisa na si kuoa tu, hata kuzaa na mwanamke mwingine. Nampenda sana mke wangu na ndiyo kwanza gari limewaka; yaani ni kama ndiyo tumekutana. Kuna wakati ninainua mikono juu kumshukuru Mungu kwa kunipa mke mwema ambaye amenizalia watoto wazuri.
OVER ZE WEEKEND: Ni kweli kwamba una ugomvi na Mondi kwa sababu alikupora Mama Qayllah?
SHETTA: Kuna vitu vingine huwa hata havina kichwa wala miguu. Kama mtu akinifuatilia kwenye Instagram mimi na Mondi, atagundua hakuna tatizo lolote.
Wakati mwingine kila mtu anaongea kitu ambacho anajisikia kuongea na hayawezi kutusababisha tuwe na tofauti. Ukiwa staa kama hivi ni kawaida na ukivisikia haviumi wala nini kwa sababu ukweli upo mioyoni mwetu.
OVER ZE WEEKEND:
Wewe na Mama Qayllah mmewezaje kudumu kwa muda mrefu?
SHETTA: Kwanza kabisa ni kuwa na mapenzi ya dhati. Pia kuvumiliana katika shida na raha. Pia kupata mwanamke wa kukuelewa na kuitambua kazi yako maana Mama Qayllah anajua vizuri changamoto za kazi yangu ya muziki.
OVER ZE WEEKEND:
Ni changamoto zipi mmezipitia kama mume na mke?
SHETTA: Changamoto hazikosekani kwenye mapenzi. Kama ni kugombana, tumeshagombana sana, lakini mwisho wa siku unaona kabisa huyu ndiye wangu na Mungu ndiye amenipa, bas
Tags