Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa kupitia JamiiForums imeeleza huduma za usafiri wa treni za abiria na mizigo kwa reli ya kati zimesitishwa
Hii ni kutokana na uharibifu wa njia ya reli uliosababishwa na mafuriko maeneo ya Kilosa, Igandu, Dodoma na Makutupora
Imefafanuliwa kuwa mvua zinazoendelea kunyesha Ukanda wa Kati zimeleta uharibifu mkubwa katika njia ya reli hasa maeneo ya Kilosa (Morogoro), Gulwe (Mpwapwa), Igandu, Zuzu na Makutupora (Singida)
Maeneo 26 yameathirika kati ya hayo 10 yako katika hali mbaya ambapo tuta la reli na baadhi ya Makalavati yamesombwa na mafuriko
TRC imeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kujaza vifusi katika maeneo yaliyoathirika kuanzia Kilosa hadi Igandu ili kurudisha mawasiliano katika maeneo hayo
NB: Picha si halisi kwa habari hii