Shirikisho la Mpira Duniani FIFA, Kuanza Kuwalipa Mishahara Wachezaji Wasiolipwa na Timu zao


Shirikisho la Soka Duniani FIFA na umoja wa wachezaji FIFPRO unaandaa mfuko utakaosaidia kuwalipa wachezaji wasio na mishahara na wale ambao hawapati mishahara pindi klabu zao zinapopitia changamoto za kiuchumi.


Hiyo imekuja kufuatia muendelezo wa klabu nyingi duniani kuporomoka kiuchumi, ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jumla ya klabu 20 duniani zimeanguka kiuchumi na kukwamisha mamia ya wachezaji.

Mfuko huo utazisaidia kulipa mishahara klabu klabu zilizoporomoka kiuchumi huku zikiwa zinafanya biashara ili zirejee katika hali yake.

SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD HAPA

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema ametenga kiasi cha Pauni Milioni 12.3 kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji ambao hawatalipwa na klabu zao kuanzia 2020 hadi 2022 huku takribani Pauni Milioni 3.8 zikitengwa kuwalipa wachezaji ambao hawajalipwa kuanzia 2015 hadi 2020.

“Makubaliano kati yetu na washirika wetu ni kuwasaidia wachezaji walio katika mazingira magumu na kazi yetu ni kuonesha uwepo wetu kama chombo kinachoongoza mpira“, amesema Infantino.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad