Upendo wangu na haupo kwake kiukweli upo kwa mdogo wake, lakini nilishindwa kuwa wake kabla ya dada yake kufanya mambo yake kweli nimeamini chelewa chelewa utakuta mwana si wako'.
Kwa jinsi nilivyompenda mdogo wake sijui ni nini kilichonifanya nisimwambie.
Nahisi ule usemi wa 'subira huvuta heri' ulinipumbaza, ona sasa kaniwahi dada yake na mdgo wake katambua.
Jamani nilimpenda na bado nampenda mdogo wake ila mazoea ya dada yake kwangu yamechukua sura nyingine.
Niliona njia rahisi ya kumpata mdogo wake ni kuzoeana na dada yake, lakini sasa dada yake kanizoea vibaya .
Hadi kufikia kuniomba namba yangu ya simu haikutosha akaamua kunitamkia kabisa eti anataka kuwa nami bila kujua kama mimi nina malengo na mdogo wake.
Nahisi ndoto zangu kupotea, nipo katika wakati mgumu sana sijui nimjibu vipi dada yake na sijui nitampata vipi nimpendae na wote wanakaa nyumba moja.
JAMANI EEH!
NIMETONGOZWA NA DADA YAKE MSICHANA NINAEMPENDA bado sijamjibu chochote nimekata mawasiliano kwa muda ili kutafakari.
Tafadhali anayeweza kunishauri.
By Alphaking mahena
je mdogo wake anakupenda?... mana waweza sema umwache dada mtu anaekupenda ukaenda kwa mdogo mtu.. ukaenda kuwa mtumwa wa Mapenz..hilo la kwanza
ReplyDelete..la pili.. wakati mdogo mtu anakuita sasa shemeji na jamii pia inatambua kuwa ww ni wa dada mkubwa.. unafikiri itakuwa ni rahisi kudumu kimapenz na mdogo mtu.. hapana mtaonekanika nyi ni wahuni mnaomdharirisha dada mtu..
..Pia hata ww si mwanaume Jasiri Mwaminifu.. unaonekanika ni mwanaume mwenye tamaa za kimwili.. ndio mana ukaanguka kimapenz.. HIVO WW HUFAI KWA HIO FAMILIA LABDA KAMA UTAAMUA KUBAKI NA DADA MTU TU
.. nakushauri tulia na dada mtu kwakuwa yy keshakupenda.. na ww mpende.. kwa mdogo mtu KAUSHAAAA
safi kabisaaa, jamaa anaonekana si mtulivu kabisa ,hafai kwenye hiyo familia ,pia dada nae utulivu ziro ,sisi watanzania atuna tamaduni ya kujirahisisha kwa mwanaume
ReplyDelete