Snura na Mpenzi Wake Minu Calypto Warudiana "Kikombe cha Plastiki Hakivunjiki kwa Kudondoka"


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi mpenzi wake Minu Calypto wameamua kuwafumba midomo wambea na kuwaonyesha kuwa wamerudiana na walivyoifaidi siku ya wapendanao.

Jana siku ya wapendanao wawili hao walionekana wakiwa na furaha na kuenjoy pamoja siku muhimu ya wapendanao katika sehemu nzuri iliyopambwa maua mekundu na baloon.

Wawili hao waliokuwa wameachana wameonyesha kurudisha mapenzi kinguvu ambapo Minu Calypo ameandika katika ukurasa wake wa kijamii "Wife❤.. Kikombe cha plastiki hakivunjiki kwa kudondoka!! I love you Snuu"

Hakuishia hapo aliendelea kumwaga maneno mtoto wa kiume ishara kuwa alikuwa anammiss pindi walipotengana na kumwambia kuwa "Hata majembe yalimayo pamoja kuna muda yanagongana.. Love❤ ".

Snura naye alijibu mapigo kwa kutupa dongo kwa wale wasiopenda kuwaona pamoja kwa kuposti picha ya mpenzi wake na  kuandika hivi katika ukurasa wake wa kijamii "Ndio kwanza nimeanza sasa sijui nnaowakera itakuaje'
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad