Steve Nyerere Mchokozi Kweli...Amvaa Tena Peter Msigwa


Msanii maarufu wa filamu hapa nchini Steve Nyerere, ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo la Iringa mjini baada ya kupokea maombi mbalimbali kutoka kwa vijana wenziye pamoja na marafiki.



Steve Nyerere ametangaza nia yake hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, ambapo ameandika.

"Iringa ya leo ni maendeleo kwanza na inahitaji vijana wachapakazi, rasmi nitagombea Ubunge Iringa Mjini ni haki yangu kurudi nyumbani, siku ya Jumatano nitakuwa na kikao cha ndani na vijana wa Iringa ahsante" amesema Steve Nyerere.

EATV & EA Radio Digital, imefanya mawasiliano na msanii huyo wa filamu na ameeleza kwa kina kwa nini ameamua kugombania Ubunge Iringa Mjini ambapo amesema,

"Nina dhamira ya kweli ya kugombania Ubunge katika Mkoa wangu, naijua vizuri Iringa kuliko watu walivyoisoma, hatutaki tena kuwatuma watumishi wazee ambao wanatafuta pesa ya pensheni, tunataka vijana wenye kuijua Iringa na lazima wanitume mtu kama mimi" amesema Steve Nyerere.

Pia ameendelea kusema "Mimi ni mkubwa najulikana nchi nzima na Afrika Mashariki yote, huwezi kunifananisha na Peter Msigwa anayejulikana mwisho Tosamaganga na Mahenge, nina uwezo na juhudi, labda aje kuniomba msamaha na anatapatapa anataka kushindana na watu na wake za watu atarudi kwenye Uchungaji".
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Steve, Wewe unapita bila kipingamizi Iringa. Leo tulikuwa Isima Vijana kwa Wazee wote Kuula zetu Unazo cha Ajabu

    Kina Mama walituuliza mna mjadili naNini na kumwagia Sifa Kemkem tukasema ni Msanii Mkubwa, Steve Nyerere..!!! Walipiga mbinja na VIGEREGEE ikimanisha Ndiye wanae kutaka UWAWAKILISHE BUNGENI.

    MZGWAANAHALI NGUMU HARUDITENA BUNNGENI JIJINI DODOMA.

    ReplyDelete
  2. Steve, Wewe unapita bila kipingamizi Iringa. Leo tulikuwa Isimani Vijana kwa Wazee, wote Kurau zetu Unazo, cha Ajabu..!!!

    Kina Mama walituuliza? mna mjadili nani, na kumwagia Sifa Kemkem..!! tukasema, ni Msanii Mkubwa!!, Steve Nyerere..!!! Walipiga mbinja na VIGEREGERE, ikimanisha Ndiye wanae kutaka UWA WAKILISHE BUNGENI.
    MsiGWA ANA HALI NGUMU, HARUDI TENA BUNGENI JIJINI DODOMA. na akija basi anakuja kununua Zabibu ili afanye mvinyo nyumbani kupoteza msongo.

    STEVE NYERERE IRINGA 2020...!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ssteve nyerere BABA LAOOOOO.
      IRINGA KAINGIAAAAA. TOKEA DILISHANI MSIGWA. KIJANI OYEEEE

      Delete
  3. Steven acha kujishaua. tunajua unapewa bichwa na wana ccm. ila Msigwa anakuangalia tu. humuwezi hata kwa Dawa Andunje wewe. ulishindwa kupanda milima KILIMANJARO utaweza ubunge..kwendraaaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Steve Ni jibu la wana Iringa.
      Tishio tosha kwa Aliyekuwa Mwakilishi mzigwa. Yeye pia anajua Ssteveana nia na wana Iringa wamtaka mchapa kazi na siyo mbishi na Mpingaji wa chama kisicho kuwa na Sera wala .... kugombania na kuminyiana mgao wa Ruzuku.

      Steve kiboko yao.. anangoja kuchukua fomu na kuanzia mwezi Machi katikati anaanza safari za mikakati ya kuchukua uwakilishi Iringa... KALAGA BAHO ..

      STEVE OYEEE..! Chungaji kachunge

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad