Taarifa Mpya Kuhusu Reli ya Kisasa



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi Desema 2019, ujenzi wa reli ya kati ya kisasa (Standard Gauge) kwa sehemu ya Dar es Salaam – Morogoro (kilometa 300) umefikia asilimia 70.


Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba, 2019.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 7, 2020) wakati akiahirisha mkutano wa 18 wa Bunge la 11 bungeni jijini Dodoma.

Amesema kazi za ujenzi kwa sehemu ya Morogoro – Makutupora (kilometa 422) zinaendelea vizuri na Serikali imerejesha huduma ya reli ya abiria na mizigo ya Kaskazini (Dar es Salaam – Moshi).

Waziri Mkuu ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuendelea na ujenzi wa Mradi wa kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere ambapo kazi zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa daraja la muda namba 2 utafiti wa miamba na udongo, uchimbaji wa mtaro wa chini kwa chini wenye urefu wa mita 147.6.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imefanikiwa kuendeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) ambapo hadi Desemba 2019 jumla ya vijiji 8,236 kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara vimeunganishwa na umeme, sawa na asilimia 67.1.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad