Taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)



Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari  03, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Ligi Kuu ya Vodacom:

Mechi namba 150: Simba SC 3 v Namungo FC  2-Mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Safisha amefungiwa miaka mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 29,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1)(a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
 
Mechi namba 157: Azam FC  1 v Mtibwa FC 1-Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa barua ya kukumbushwa  kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika mechi iliyochezwa  Januari 30,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Vile vile katika mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya Makamishina kwa kosa la kutoa taarifa yenye mapungufu.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti Kamishina
 
Ligi Daraja la Kwanza:
 
Mechi namba 75A :Friend Rangers(0)   vs Dodoma FC(1)-Kiongozi wa Klabu ya Friends Rangers Heri Chibakasa amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kupigana na washabiki wa timu pinzani
 
Ligi Daraja la Pili:

Mechi namba 29A:Dar City Fc (1) vs African Sports(0)- Mwamuzi  Salum Mkole amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kuonyesha udhaifu katika usahihi wa kutoa kadi katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 31,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1) kuhusu Udhibiti wa Waamuzi katika mechi iliyochezwa Februari 01,2020 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
 
Vile vile katika  mchezo huo mchezaji wa Klabu Ya  African Sports Rajabu Kipango amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kumpiga  mchezaji wa Timu pinzani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad