Tahadhari ya Hali Mbaya ya HEWA na Mafuriko Yatolewa Uingereza
0
February 17, 2020
Mamlaka za Uingereza zimetoa tahadhari za mafuriko kwa siku zijazo kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo
Katibu wa Mazingira, George Eustice amesema japokuwa hawawezi kumuokoa kila mtu, Serikali imewekeza mabilioni ya pesa katika miundombinu ili kukabiliana na mafuriko hayo
Mvua hizo ambazo zimesababishwa na Kimbunga Dennis zimedumu kwa takriban saa 48, zikiwa zimeambatana na upepo mkali
Japokuwa hatari ya Kimbunga hicho imepita, Wataalamu wameonya kuwa huenda hali ya mvua na upepo ikaendelea wiki hii
Kimbunga Dennis kimekuja takriban wiki moja baada ya Kimbunga Ciara kuleta madhara makubwa katika baadhi ya maeneo ya Uingereza
Tags