TAHARUKI imetanda katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro,baada ya kuanza kuonekana makundi madogo madogo ya nzige.
Nzige hao, wameonekana vijiji vya Korini, Kata ya Mbokomu na Mwasi Kata ya Mwika Kusini.
Wakizungumza baadhi ya wakazi wa Kijiji Cha Korini,walisema nzige hao walianza kuwasili saa 10 jioni, Februari 8, mwaka huu wakiwa katika maukundi madogo madogo.
Mkazi wa kijiji hicho, Gladness Mchau alisema nzige waliingia kijijini saa 11 jioni na kuzua taharuki kubwa, huku wakiofia huenda wanatoka nchi jirani ya Kenya ambako waliripotiwa kuingia na kuvamia mashamba mwezi uliopita.
“Nzige wakuja juzi jioni wakiwa wengi sana, jambo ambalo lilitusangaza,hatujawahi kuwaona kabisa machoni,na tuliofia huenda ni wale wa Kenya, hasa ukizingatiwa tupo karibu hapa.
“Ni waajabu waliingia wengi kiasi kwamba sikuweza kujua wako wangapi haraka haraka, wanaonekana kuweka kivuli chini na baada ya jua kuwaka sana walikimbia na mpaka sasa unawaona hapa mmoja mmoja na ndege wanawala,”alisema.
Eliaringa Mcharo,alisema baada ya kuona nzige hao watoto walianza kuwaangamiza kwa lengo la kuwafanya vitoweo, lakini waliwaambia wasiwale kutokana.
“Watoto waliwavamia na kuwaua kwa lengo la kuwageuza kitoweo, niwaambia wasiwale huenda wakawa na sumu ….tulimtafuta ofisa ugavi ili atusaidie kiwatambua kwa bahati mbaya hatukumpata,”alisema.
Alisema ni vema Serikali kwa kutumia wataalamu wake wa kilimo kufika kijijini hapo na kuwatambua kama ndio wenyewe ili hatua za kuwathibiti zichukuliwe, ikingatiwa sasa ni msimu wa kuandaa mashamba kwaajili ya kilimo.
“Msimu huu, unavyoona tunaanda mashamba,kama ni wenyewe ni hatari na huenda kukawa na njaa, tuliona Kenya namna walivyo haribu mashamba,”alisema.
Ofisa Kilimo Wilaya ya Moshi, anaye husika na afya ya mimea, Gudluck Tito alithibitisha kuwapo nzige.
Alisema nzige hao, ni jangwani kulingana na mafunzo waliopewa ya namna ya kuwatambua tena wenye sifa ya kuharibu mazao mashambani.
“Tupokea taarifa kuna panzi waofanana na nzige ambao nimewaambia,wanaonekana kufanana na nzige ila taarifa rasmi itatolewa na wataalamu wa kanda ya kaskazini,”alisema.
Alisema amepata taarifa za uwapo wa nzige katika mipaka ya Kenya na Wilaya ya Moshi, wameonekana vijiji vya Korini na Mwasi.
Alisema mpaka sasa Serikali imeanza kuchukua kukabiliana nao,ikiwa ni pamoja na kununua sumu zaidi ya lita 7,000 na kuagiza ndege maalumu ya kunyunyuzia dawa.
“Tayari Serikali imeanza kuchukua jitihada ambapo zaidi ya lita 7,000 zimenunuliwa pamoja na kuagiza ndege za kunyunyuzia dawa ili kukabiliana nao ili wasiingie nchini kirahisi,” alisema.
Mratibu wa Kituo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kaskazini, Mwinyi Mkuu alithibitisha uwapo wa nzige hao na kusisitiza yeye si msemaji aulizwe mkurugenzi wake, lakini juhudi za kumpata hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni.
TAHARUKI imetanda katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro,baada ya kuanza kuonekana makundi madogo madogo ya nzige.
0
February 10, 2020
Tags