Tanzania Kitovu cha idadi ya Simba Duniani


Tanzania imetajwa kuwa ni kitovu cha Simba duniani kwa kuwa na Simba kati ya asilimia 40 na 50 ya wanyama hao katika hifadhi zake.

Akizungumza jana kabla ya kuanza kuwahamisha simba 17 kutoka ikolojia ya Serengeti mkoani Mara kwenda hifadhi ya Taifa Burigi mkoani Geita, mtafiti wa simba kutoka taasisi ya utafiti ya wanyama pori (Tawiri), Dkt. Ikunda amesema pia idadi ya Simba waliopo Tanzania, asilimia 50 wanapatikana katika ikolojia ya Serengeti na imesababishwa na mamlaka husika katika hifadhi hiyo kuhakikisha kuna uhifadhi endelevu katika hifadhi hiyo hali iliyopelekea waanze kupunguza simba hao.


” Kutokana na ongezeko hilo, mamlaka husika zimeamua kuwahamisha baadhi ya simba katika hifadhi ya Taifa ya Buringi ambako kuna idadi ndogo ya wanyama hao” amesema Dkt. Ikunda.

Amebainisha njia waliyotumia kuwaandaa ikiwa ni pamoja na kufungiwa katika boma maalumu kwa zaidi ya siku 20.



” Kwavile kule Burigi kwa mujibu wa utafiti chakula kikuu ni pundamilia, baada ya kuwakamata tumekuwa tukiwapa nyama ya pundamilia ili wakifika kule wasipate shida, wawe wamezoea kwahiyo hatuna wasiwasi tayari wamesha zoea hali hiyo” ameeleza Dkt. Ikunda.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ( senapa), Misana Mwishawa amesema lengo la simba hao kuhamishwa Buringi ni kutaka kuboresha na kuimarisha utalii katika hifadhi hiyo na nchi kwa ujumla.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad