Tanzania Yashika Namba 73 Duniani Kwenye Passport zenye nguvu


Tanzania ipo kwenye 100 bora ya Nchi ambazo Passport zake zina nguvu duniani ikishika namba 73, kwa Afrika imezipita Nchi mbalimbali ikiwemo Uganda (77), Ghana (78), Morocco (80), Rwanda (83), Nigeria (95), Congo DRC (94), Zimbabwe (79).

Top 5 ni Luxembourg na Spain zimefungana kwa passport zao kuwa na uwezo wa kumpeleka Mtu Nchi 187 bila VISA au VISA wakapatiwa wakati wa kuwasili, kwa ufupi ni kwamba Nchi hizi zimewaondolea Raia wake usumbufu/mlolongo wa kuomba ruhusa ya kuingia Nchi nyingine (VISA) ambayo huchukua muda wakati wa kuomba na wakati mwingine wengine hunyimwa VISA hizo.

Namba 4 ni Italy na Finland, (Nchi 188), namba tatu ni South Korea (Nchi 189) huku Singapore ikishika namba mbili kwa kufikisha Nchi 190, Japan ndiyo namba moja kwa Nchi 191.

Mataifa maarufu ambayo hayapo Top 5 ni pamoja na Marekani na Uingereza ambao kwa pamoja wameshika namba 8 (Nchi 184), Canada na Australia namba 9 (Nchi 183), United Arab Emirates namba 18 (Nchi 171), Brazil namba 19 (Nchi 170), Israel namba 25 (Nchi 159) na Russia ambayo imeshika namba 52 (Nchi 118)

SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD HAPA

South Africa imeshika namba 56 (Nchi 100), kwa upande wa idadi ya Nchi zilizotajwa kwa Tanzania ni 70 ambapo haipo mbali sana na China iliyoshika namba 72 (Nchi 71).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad