TRA Kilimanjaro yakamata mapipa 50 ya 'spirit' yakisafirishwa kwa magendo kwenda kenya



Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa wa Kilimanjaro imeendelea na operesheni dhidi ya biashara za magendo mipakani ambapo imekamata mapipa 50 yenye jumla ya  lita 12,500 za kemikali (spirit)  yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 15.5 ilyokuwa ikisafirishwa kwenda nchi jirani ya Kenya.

Akizungumza na  wanahabari leo february 26.2020 ,Meneja Mamlaka ya mapato Mkoani wa Kilimanjaro,Gabriel  Mwangosi amesema mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti upitishwaji wa  biashara za magendo  zinazoingizwa na kutolewa nje ya mipaka kwa kutumia njia zisizo rasmi na kwamba wamejipanga usiku na mchana kuhakikisha vitendo hivyo vinadhibitiwa kikamilifu.

Amesema katika operesheni hiyo wamekamata pia simu  1076 za viganjani aina ya Itel zenye thamani ya zaidi ya sh14.8 milioni katika mpaka wa Holili uliopo Wilaya ya Rombo zilizokuwa zikiingizwa nchini kinyume na sheria.

Mwamgosi amesema bidhaa zote na magari yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa hizo yanashikiliwa na mamlaka hiyo huku taratibu za kisheria zikiendea kuchukuliwa juu ya uvunjifu huo wa sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad