Ikulu ya Marekani yatoa Taarifa Rasmi ya Sababu za Kumuua Kamanda wa Jeshi la Iran.....Baraza la Seneti Lapitisha Sheria Kumzuia Trump Kuishambulia Iran



Ikulu ya Marekani jana imetoa taarifa  ikisema Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru shambulizi la droni lililomuua kamanda mkuu wa jeshi la Iran mwezi uliopita ili kujibu mashambulizi ya nyuma, licha ya madai ya awali kwamba yalitokana na tishio la hivi karibuni.

Kama inavyohitajika kisheria, serikali imetuma taarifa kwa baraza la chini la bunge la Marekani ikielezea shambulizi la Januari 2 lililomuua Qasem Soleiman katika uwanja wa ndege wa Baghdad.

 Shambulizi hilo na jibu la Iran yamezua wasiwasi na kufadhaisha baadhi ya wabunge ambao walisema Trump alifanya kosa kubwa na amewapa Wairan haki ya kushambulia.

Siku moja baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo kwa baraza la congress, kamati ya mambo ya nje ya baraza la chini la bunge la Mrekani, imekemea kitendo  hicho cha Trump, na kupitisha  muswada wa sheria ya kuweka ukomo juu ya uwezo wa rais wa kuendelea na vita dhidi ya Iran.

Baraza hilo limepitisha mswada huo kwa kura 55 za ndiyo na kura 45 za hapana, huku wanachama 8 wa Republican wakipiga kura za ndiyo.

Muswada huo umesisitiza kuwa rais Trump hawezi kuchukua hatua za kijeshi bila ya ridhaa ya bunge.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad