Tyson Fury Amuomba Wilder Akubali yaishe tu



Bondia muingereza Tyson Fury baada ya kushinda Ubingwa wa Dunia uzito wa juu kwa TKO kwa kumpiga Deontay Wilder round ya 7 na kubeba mkanda wa WBC, awali ilikuwa inafahamika kuwa Bingwa wa pambano hilo la marudiano baada ya awali kutoka sare ataenda kupambana na bondia Anthony Joshua.

Kutokana na sheria ya mkataba waliosainishana Tyson Fury na Deontay Wilder unawataka kurudiana kwa mara ya tatu kama Wilder atapenda kitu ambacho inaaminika kuwa hawezi kukataa kurudiana nae, sasa inadaiwa kuwa upande wa Tyson Fury promota wa pambano hilo Frank Warren amepanga kumshawishi Wilder kwa pesa ili aachane na ishu za kurudiana na Fury na badala yake lipigwe vs Anthony Joshua.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad